Huyu mwanadada member wa JF napenda sana tabia yake

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Posts
27,970
Reaction score
35,168
Mie sijambo kama nyie.

Nasema kutoka moyoni tena bila kushuritishwa na mtu, napenda sana tabia ya huyu dada member mwenzetu hapa JF. Huyu dada hana maringo, hana hasira hata mtu akimjibu utumbo. Hivi kwa nini na mie sina tabia njema kama za huyu dada (nina hasira sana). Mie mtu akinitibua ni jino kwa jino, jicho kwa jicho, mguu kwa mguu, mkono kwa mkono kinachofuatia ni nasomeka BANNED.

Wewe dada una busara sana. Mimi kama mwanamke mwenzio nasema hivi una tabia njema. Na kama una familia basi familia yako utakuwa unawalea katika maadili mazuri.

Huwa nikiona mtu "anamchokoza" huyu dada niko tayari kuingilia huo ugomvi (nina element za ugomvi sipendagi ujinga mimi).

Barikiwa sana Dada Sky Eclat pia nakutakia maandalizi mema ya mfungo (Kwaresma).
 
Shukran mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…