Huyu mwanafunzi nimeshindwa kumwelewa

Huyu mwanafunzi nimeshindwa kumwelewa

Brightman Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2009
Posts
1,224
Reaction score
234
Wakuu leo nikiwa katika nyumba ya ibada kumwabudu Mungu nimeshangaa na kushindwa kumwelewa mwanafunzi mwenye matokeo haya:

S2663/0001
F
34
FLD
CIV-F HIST-F GEO-F KISW-D ENGL-F PHY-F CHEM-F BIO-F B/MATH-F


alipopita mbele na kutoa shukrani kwa Mungu kwa matokeo hayo. Nimetafakari sana nimeshindwa kupata majibu. Hii imani ni kubwa kiasi gani? Wangapi wenye matokeo kama hayo waliotoa sadaka ya shukrani kwa Mungu!
 
Shukuruni katika kila jambo. Huyo yuko katika hatua ya kuaccept na akitoka hapo ataendelea na maisha. Ambao hawakukubaliana na matokeo wamejiua!!


Sent from my iPhone
 
Hio ndio imani inayotakiwa mungu atamsaidia atafikia mlengo tu kila mwenye imani atafanikiwa anavyoamini.
 
wewe kama umemshangaa basi wewe unaonekana zombi kwani imani inatuambia tushukuru kwa kila jambo hata kama ni baya sasa wewe inabidi utuambie kwa nini umshangae
 
kwi kwi kwi nimecheka mbaya ndo maana ulokoleni sio kuzuri kuchagulia mchumba kule kumejazana watu wenye stress sana na kukata tamaa.

umecheka kwa lipi? shukuru kwa kila jambo ndo maana watu huwa wanapoteza baraka za MUNGU
 
Zawadi , Fofader na mipango mmenipa mwanga kwakweli huu ni ujasiri mkubwa ameonesha huyo binti!
Upande wa KALEBE mie sijakuelewa hivi zombi ni mnyama gani?
 
Last edited by a moderator:
Mungu atasingiziwa mengi sana mwaka huu.

Huyu anashukuru "kufaulu" kwa sababu katika vitabu vya NECTA, kufeli ni division 0.
 
We ungekuwepo siku ile mjane alipotoa sadaka ya sent tano aliyekua anaetegemea kwa msosi, ungechekaje?!
 
We KILANGA umeona vizuri hayo matokeo! Ebu mtoto niingie kwenye desktop nikupe LIKE...!
 
Last edited by a moderator:
kwi kwi kwi nimecheka mbaya ndo maana ulokoleni sio kuzuri kuchagulia mchumba kule kumejazana watu wenye stress sana na kukata tamaa.
Stress sio za walokole ila ni maumbile ya kibinadamu,hakuna ambaye hana au hajawahi kuwa na stress,Bill Gates mwenyewe ana stress itakuwa wewe mla vumbi wa ulimwengu wa tatu!
 
Nimezifurahia comment zenu nyie watu. Kumbe ni muhimu kumshukuru Mungu kwa kila jambo!
 
Mungu atasingiziwa mengi sana mwaka huu.

Huyu anashukuru "kufaulu" kwa sababu katika vitabu vya NECTA, kufeli ni division 0.

Mkuu Kiranga, sijui kwa nini serikali ikaweka division 0 pekee ndiyo kufeli maana ukiangalia kwa makini division 4 zingine ni huko huko tu kwenye 0!!
 
Ana akili sana huyo binti " mshukuru Mungu kwa kila jambo" nina imani ana Amani na faraja kubwa na Mungu atamsimamia,, Kufeli shuleni sio kufeli maisha

Mnaocheka endeleeni kumcheka ipo siku mtamuelewa,,, malipo ni hapa hapa duniani
 
Back
Top Bottom