Huyu mwanamke itakua anaumwa ugonjwa gani ?

Huyu mwanamke itakua anaumwa ugonjwa gani ?

Sensei Tai

Senior Member
Joined
May 26, 2022
Posts
168
Reaction score
466
Kuna mwanamke mmoja nipo nae kwenye mahusiano na huwa tutakutana kimwili mara mbili au mara tatu kwa mwezi.

Mara nyingi tukikutana huwa hatutumii kinga sababu wote tulienda kupima kipimo kikubwa na kuonekana wote damu zetu zipo safi kwamaana hatuna maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Wiki mbili zilizopita nikutana nae kimwili lakini baada ya siku mbili tatu nikaanza kuhisi nawashwa kwenye njia ya mkojo na napata tabu kujikuna mana hata ukikuna ngozi bado muwasho hauondoki mana upo kwenye njia ya mkojo.

Hapa jirani kuna duka la dawa anauza mama flani sasa nilienda nikamuelezea kisha akanipatia dawa ya kutumia siku tano na kweli baada ya kutumia lile tatizo likaisha.

Sasa ombi langu kwenu wataalamu nataka mnijuze kulingana na maelezo yangu huu ugonjwa ni ugonjwa gani, mana sina mwanamke mwingine zaidi yake ambae nasex nae hivyo yeye ndie ambae aliniambukiza huu ugonjwa kwa asilimia 100%.

Wataalamu naomba mnijuze kulingana na uzoefu wenu wa masuala ta magonjwa

Ahsante
 
Acha ujinga wewe. Utakufa

Ugonjwa sio HIV. Hivyo kumkuta hana hiv haimaanishi na magonjwa mengine hana.

Kuna homa ya ini ni hatari kuliko HIV.

Kuna kansa za kizazi HPV nazo zinaambukizwa kwa ngono.

Na Kuna magonjwa mengine zaidi ya 100 yanaambukizwa kwa ngono
 
Wote tulienda kupima kipimo kikubwa na kuonekana wote damu zetu zipo safi kwamaana hatuna maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Magonjwa hatari siyo UKIMWI pekee ila ingawa wapenda ngono huwa mnawaza gonjwa moja tu, lakini kuna :-
1. Hepatitis / homa ya ini
2. Syphilis / kaswende

Haya magonjwa ni hatari sana kwa binadamu..

Sasa ombi langu kwenu wataalamu nataka mnijuze kulingana na maelezo yangu huu ugonjwa ni ugonjwa gani, mana sina mwanamke mwingine zaidi yake ambae nasex nae hivyo yeye ndie ambae aliniambukiza huu ugonjwa kwa asilimia 100%.

Huwezi kujua ugonjwa wa mwanamke bila yeye kutoa maelezo yaliyo kamilika.
Labda yawezekana anatatizo la
1. Fungus
2. PID.
 
Hapa hautapata majibu sahihi

Ila ni vizuri ukaenda nae hosptalini ili mpime STI -magonjwa ya zinaa .

Kwa kufanya hivi utakuwa umejiweka sehemu salama zaidi

Maana gharama za kutibu magonjwa zipo juu na njia ya kukabiliana na hizo gharama ni kuijali Afya yako .
 
PID hiyo.Inawasumbua wanawake wengi Sana kwa sasa.Mara nyingi wakipima maabara huaminishwa ni Fangasi na UTI sugu,wanatumia antibaktria ugonjwa unatulia huku ukiendelea kukua.
 
Acha ujinga wewe. Utakufa

Ugonjwa sio HIV. Hivyo kumkuta hana hiv haimaanishi na magonjwa mengine hana.

Kuna homa ya ini ni hatari kuliko HIV.

Kuna kansa za kizazi HPV nazo zinaambukizwa kwa ngono.

Na Kuna magonjwa mengine zaidi ya 100 yanaambukizwa kwa ngono
Wamekalili HIV tu ndiyo ugonjwa hatari,. Kuna kaka mmoja mama yake alikuwa na kisukari alisema Bora mama angekuwa na HIV ningekuwa namhudumia kuliko sukari, mpaka sasa alishamzika miezi 7 iliopita.
 
Back
Top Bottom