Huyu mwanamke ni sahihi kuniambia maneno haya?

Abdul Mganyizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2019
Posts
1,040
Reaction score
2,010
Habari za harakati za maisha wananzengo,

Niiende kwa hoja moja kwa moja. Nina mke wangu ambae leo tunamiaka mitatu kasoro. Tumekuwa tukiishi vzr tu bila ugomvi na kama upo ile kupishana tu kauli.

Sasa kabla ya chirismas nilipanga safari ya kwenda mkoani Kagera, nikanunua mahitaji yote mf mchele, unga, mafuta, sabuni, ngano, maharage na vitu vingne ambavyo ni mahitaji.

Safari yangu ilikuwa ni ya week moja ambapo niliondoka j'2 na kurudi J'3 ya week iliyofuata. Sasa pesa za matumizi ya mboga ,labda mshumaa In case umeme umekata nilimpa shilingi 30,000.

Ndani wapo watu watatu mke wangu, mjomba wangu yaani mtoto wa dadaangu yupo form one na mwanangu mdogo ana mwaka mmoja na nusu.

Kabla ya siku mbili kuanza safari ya kurudi alinipigia simu anasema pesa imeisha ya matumizi, mwanamme mzima naiachia familia nzima elf 30000 kwa muda wa wiki nzima ,kwakweli nikaumia sana kwa maneno yale. Lakini kubwa zaidi nilivyomuambia kuwa anivumilie kwesho kutwa nakuja akasema bora hata upate ajali ufie huko usirudi kabisaa make mme gani huwezi kulea familia.

Mm kipato changu ni shiling laki tano kwa mwezi ila ninavyoona mke wangu anahitaji maisha ya kupato cha milioni. Maneno anayoniambia kama huwezi kulea familia subiri uje usaidiwe yamenikasirisha sana wakati mm ninatoa kile nilicho nacho.

Sasa ndugu zangu mwanamke kama huyo utamfanyaje?
 
Kuna mwamba anaanza kumnyatia.
 
Hela ndogo hiyo miharage watakula kila siku eeh?

Siku saba dagaa anunue kiasi gani na aziunge ili zilike vizur na nyama hajanunua. Acha ubahiri ukiona mkeo kakuchoka na ukute sokoni unaenda mwenyewe unajiona mwamba kununua mivyakula hiyo. Mpe pesa mkeo apambane mwenyewe na bajeti zipo za bei ndogo ila unabadilisha mlo.
Mindondo kila siku sio mchezo we jamaa
 
Kwanza unatakiwa kujua akili ya mwanamke haina akili, kesho ukimuuliza alicho kisema leo atakana kusema hakusema hivyo au msamehe shetani alimpitia.

Pili uje mtu huzungumza kilicho moyoni mwake, hivyo hayo aliyo sema tarajia yatatekelezeka sio muda mrefu.

Mwisho chukua tahadhari za kiume, ukiweza mshutue na makofi kidogo ili awe na tahadhari na kauli na matendo yake juu yako.

Mwisho wa yote ndugu mwanamke usimzingatie sana, angalia maisha yako na watoto wako , usimpe mwanamke moyo wako wote, mpe asimilia ndogo sana, au ikibidi usimpe kabisa.
 
Wengi katika watu tukipata huwa twawa wanafiki na kujifanya tumeyasahu misha ya watanzania waliyo wengi kwelikweli

Naam, kweli kwa usawa ya maisha ya sasa ni pesa chache sana, lakini ndio aliyokuwepo nayo mume, na mke apaswa atambue kipato cha mumewe

Sasa ukiitisha iko kikubwa ambacho mumeo hana, akaibe??

Mbaya ni mume kukaa nyumbani kunyoosha miguu asitoke kwenda kutafuta, au anaafuta ila anatumia kwa njia zisizofaa au analeta ubahiri, ila hii ya kupata kisichotoshea haifai kumfarikisha kwahiyo atoe wapi??? Kama huwezi achika kaolewe pahala zipo(kama ndio solution uionayo)

Mshahara wenyewe sijui profit kasema ni kipato cha laki tano pengine ukute nyumbani kwao yeye ndio basa aya wategemea nini hapo???

Labda kuwe na makandokando mengine ila kama sivyo huyo mke mwenyewe adabu hana hadi akuombea kifo duuh, kazi kwelikweli

Wana jf baadhi comments zao huwa utafikiri wao wana dunia yao nyingine kabisaa sio dunia hii ya Mimi na wewe

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Mwambie huyo
Wape ile story yako na mwiraq wako mkuu
 
JF kila mtu humu ni tajiri. Yaani mahitaji yote ya msingi yamo ndani mfano unga, mafuta, sabuni, mchele, maharage, mkaa,luku, nk. Halafu elfu 30 kwa wiki haitoshi???

Operation kataa ndoa acha iendelee tu hakuna namna. Kwa coments hizi nakushauri achana tu na huyo mke wakokumbe hakuna la maana unalolifanya kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…