Huyu ndie bilionea namba moja Tanzania

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji (39), ametajwa kuwa ndiyo bilionea namba moja nchini kwa sasa, akifuatiwa na Rostam Aziz (49).

Kwa mujibu wa ripoti ya Jarida la Ventures Afrika lililotolewa jana, wafanyabiashara hao ndiyo Watanzania pekee waliongia kwenye orodha ya mabilionea 55 barani Afrika.
Dewji, ambaye
pia

ni mbunge wa Singida Mjini kwa tiketi ya CCM, ni mfanyabishara kijana aliyekamata nafasi ya 24 katika orodha hiyo akiwa na utajiri wa Dola 2 bilioni Marekani (Sh3 trilioni). Nafasi hiyo inamfanya kijana huyo kutambulika kama tajiri namba moja nchini kwa sasa na siyo tena Rostam.

Katika orodha hiyo Dewji amemwacha Rostam kwa nafasi 16. Rostam anashika nafasi ya 40 akiwa na utajiri wa Dola 1.2 bilioni za Marekani.

Mwaka jana, Rostam alitajwa kuwa ndiye tajiri namba moja Tanzania. Hiyo ilikuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na jarida la Marekani la Forbes. Rostam alikamata nafasi hiyo na ya 27 katika Afrika akiwa na utajiri wa Dola 1 bilioni za Marekani (Sh1.6 trilioni).
Katika orodha hiyo, yumo pia Said Bakhresa ambaye aliwahi kutajwa siku za nyuma kuwa mmoja wa mabilionea wa Tanzania na Afrika.

Hata hivyo, ripoti ya jarida hilo ya mwaka 2011, ilimtaja Bakhresa kuwa ndiye aliyekuwa tajiri namba moja wa Tanzania. Bakhressa katika kipindi hicho alikadiriwa kuwa na utajiri wa Dola 620 milioni (Sh971 bilioni) akifuatiwa na Rostam, Mengi na mfanyabiashara mwingine maarufu, Ali Mufuruki.

Mengi alishikilia nafasi ya pili Tanzania na 34 Afrika akiwa na utajiri wa Dola 550 za Marekani (Sh861 bilioni).
Forbes ilionyesha kuwa Bakhresa alifungana na Mo katika nafasi ya tatu ya orodha ya matajiri wa Tanzania na ya 38 kwa Afrika. Wote walikuwa na utajiri wa Dola 500 milioni (Sh783 bilioni). Jarida hilo limemtaja pia tajiri

kijana wa Nigeria mwenye umri sawa na Dewji, Igho Sanomi kuwa anashika nafasi ya 30 akimiliki Dola 1.3 bilioni.chanzo.
http://kwetufashiontz.blogspot.com.tr/2014/11/huyu-ndie-bilionea-namba-moja-tanzania.html
 
Hiyo ni kutafuta sifa tuu ukweli ni kuwa Bakhresa ndiye tajiri namba 1 tanzania.Amewekeza msumbiji,malawi,rwanda,uganda burundi na muda sii mrefu atafungua viwanda kenya.Bakhresa anatoa ajira zinazoonekana,bidhaa zinazotomika kila siku,kodi analipa hana madeni bank za ndani.Wakati METL ndiye mdaiwa mkubwa stanbic,ana viwanda alipewa PSRC mpaka leo hajaviendeleza amefanya goodown
 

Mo Dewji alinunua karibu mashamba yote ya Mkonge ya serikali, pia alinunua kiwanda na mashamba ya Chai Tukuyu, Mbeya. Ukifanya evaluation ya hiyo ardhi thamani yake ni zaidi ya hizo tulizotajiwa...

Mi kinachonishangaza ripoti za Forbes haziko consistent, mtu mwaka jana alikuwa na m550 Leo ana 2b baada ya mwaka
 
Ni mbunge wa Tabora na ni bilionea, right? So tell me how many good hospitals does Tabora have? How many good schools? I mean he should be able to invest some of that money to ensure that the people who elected him are never forced to travel to Muhimbili or KCMC or private hospitals in Dar or Nairobi or India for a better hospital.
All these so called milionnaires/bilionaires and in government positions are just rubbish. He is 39 can we please be told how he got his wealth? Including Rostam Aziz?
 
Maskini Rostam anazidi kuporomoka, wasingemfanyia siasa za maji taka sasa hivi angekuwa juu zaidi....
 
Huyu dewji nae sie huyu
ni msaniii
shughuli zake hazieleweki ni mwana siasa?
Vitu alivyochukua psrc mbona viko vilevile?
huyu nakataaa sio tajiri.ni mpenda sifa
 
Hapo kwenye red baba unamzungumzia Madeni Maharage ? Naye ametajwa kuwa ni billionea?
 
Kuna jamaa mmojaalikuwa anacheza bao huku anapiga miayo siku mbili hajala kitu cha kueleweka mfukoni yuko tee anajadili mabilioni ya dola.
 
Nani tajiri zaidi ya mwenzake kati ya Mohammed Gulam Dewji na Gulam Mohammed Dewji. Hawa watu ni mtu na mtoto wake. Mtoto ni CEO wa METL na Baba ni Chairman wa METL. Watafiti wanatuchanganya kila kukicha, leo watasema Mohamedi ni tajiri na kesho wanasema Gulam ni tajiri lakini mali inayozungumziwa ni ile ile makampuni ya METL.
 

hili nalo neno!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…