Huyu ndio Ibrahim Pasha wa Tamthilia ya Sultan

Joined
Jul 22, 2018
Posts
18
Reaction score
46

Huu ndio wasifu wa Ibrahim Pasha anayeigiza katika Tamthilia ya Sultan kupitia King'amuzi cha azamtvtz ndani ya chaneli ya Azam Two.

Jina lake halisi ni Okan Yalabik.alizaliwa tarehe 13/12/1978 katika mji wa Istanbul - Uturuki.

Ni muigizaji msomi mwenye shahada mbili za masuala ya sanaa. Shahada yake ya kwanza alihitimu katika chuo cha Istanbul University State Conservatory na ya pili alihitimu katika chuo cha Kadir Has University.

Alianza kutambulika rasmi katika ulimwengu wa filamu mwaka 2001 na mpaka sasa ameigiza Filamu na Tamthilia zaidi ya ishirini ikiwemo Tamthilia pendwa ya Sultan.

Ndani ya sultan ameigiza kama Ibrahim Pasha ( İbrahim Paşa) akihudumu kama Waziri Mkuu,Mkuu wa Usalama, Msaidizi na Swahiba wa Sultan Suleiman(Mtukukufu) wa Himaya ya Ottoman.

pia ameigiza kama Mume wa dada yake Sultan Suleiman anayefahamika kwa jina la Hadije Sultana.

Sambamba na uigizaji wa filamu na Tamthilia, Okan ni muigizaji mzuri wa maigizo ya jukwaani(Theater), pia ni msanii wa kuigiza sauti (Voice Over Artist).

Mwaka 2008, 2011 na 2016 aliigiza sauti katika mfululizo wa Filamu za Kung Fu panda zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kituruki.

Asante kwa kutenga mda wako kusoma makala hii.like, comment, share ila tafadhali usisahau kumtaja au kumtambua muandishi wa makala ambaye ni mimi jamvini storyteller. nitakushukuru kwa uungwana wako.

nimeiandika kwa msaada wa vyanzo mbalimbali toka kwenye mtandao.

karibu.

JamiiForums - Where we Dare to Talk Openly
 
seneta acha masihara pls.[emoji23]

pasha ameweka kibindoni degree mbili za masuala ya sanaa.

huyo gabo ukiondoa zile mbwembwe za nahau na misemo yake ya kiswahili iliyojaa ujanjaujanja, ana nini cha zaidi?.
[emoji121]
HUWEZI KUMFANANISHA JINIAZI GABO_ZIGAMBA NA WAPIGA POROJO WENGINE ETI KISA WANA SHAHADA MBILI,

KIPAJI NI ZAIDI YA SHAHADA.
 
Ahsante sana ndugu storyteller kwa wasifu wa bwana Theo aka mtumwa kutoka Pargal...

Ila ingependeza kama ungeongeza baadhi ya vitu kama..

Maisha binafsi (familia)

Mafanikio aliyopata kupitia tamthilia ya SULTAN{magnificent Century}
 
Tz waigizaji wengi Std 7 na fm4 failure hafu tutegemee wataigiza kama waturuki, au wakorea au waphilipino, nazani Sana'a ya Tz haitakuja kukuwa.
 
Ila yule commedian fulani sijui Sambua anaitwa, ni chizi balaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…