Huyu ndiye binti wa Mwl Mwakasege ambaye ni mmoja wa marubani aliyerusha ndege iliyobeba mwili wa Rais Magufuli

Malezi makini ya wazazi kwa watoto na miongozo sahihi ni nini tosha. Mambo ya familia kuwa na pesa ni secondary. Kuna mabillionnaire ila watoto wao hawana tofauti na chokoraaa na mifano ipo. Hongereni sana mwalimu Christopher Mwajasege na Diana Mwajasege.

Pia majina ya kuwapa watoto muwe nayo makini. Nimegundua majina ya Anna ni miongoni mwa yenye bahati na wapambanaji sana.
 
Wanawake huu ni mwaka wenu wa kujimwambafai. Siku za nyuma mlikuwa mnatusumbua na nyimbo zenu eti wanawake tunaweza huku hakuna mifano ya kutuonyesha.

Mbali na huyo Rubani pia Rais wetu wa nchi nae ni Mwanamke, pia wapo Mawaziri na wakuu wa Mikoa na wilaya. Hata kwenye michezo yupo CEO wa timu ya Simba wote hao wanasafisha njia kwa wengine kuwa wakipewa nafasi - wanaweza.
 
watu bwana, mnaanza kuingiza mambo ya dini.......hapo swala ni kwamba baba anaweza kumsomesha.....wa ngapi walikuwa na maono lakini hawakufanikiwa kwa kukosa pesa.....
 
Urubani hauhitaji akili nyingi.
Ukiwa na mambo 3 tu inatosha.
1. Pesa
2. Utimamu wa akili na mwili
3. Lengo.
Hata ukipata form form D tatu ikiwemo angalau moja ya mathematics au physics inatosha. Ukiwa maskini sahau urubani maishani mwako hata upate A masomo yote, labda utapaisha ndege za jeshi tu
 
Huo ndio uzuri wa wwzazi kuombea ndoto za watoto.
Wengi hatujatimiza ndoto zetu sababu shetani na majeshi yake wamezinyakuwa, hatukuwa na wa kutuombea
kula kimasihara sana kuna athiri sana mambo ya ndoto, haswa katika ulimwengu wa roho
 
Nilisoma kuwa huko US marubani hulipwa hela kiduchu hadi wengine wanafanya kazi mbilimbili. Huo hii kazi imekuwa ya kawaida sana. Sema kibongobongo bado ni kazi adhimu.

Halafu kuna kujifunza kurusha zile ndogo kama za michezo au za kunyunyiza dawa, hata miezi sita haifiki unaitimu.
 
Ndo nawashangaa hawa Majuha. Urubani hata kama form four hujapata cheti kuna baadhi ya vyuo wanakuchukua baada ya katest kadogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…