Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi ni kipi kinaleta muwasho ukajikuna vipele vikakutoka? uataka kuniambia ni maelezo yako ndiyo hupelekea hivyo pia?Si kweli Mkuu kwa hoja zifuatazo:-
Chunusi (Acne Vulgaris) ni ugonjwa unaohusisha tezi za kuzalisha mafuta (oil glands) zilizopo chini ya ngozi kwenye sehemu ya vijitundu vya vinyweleo (hair follicles)
Kila kitengo huundwa na kijitundu cha kinyweleo (hair follicle), tezi ya mafuta (sebacious gland) na kinyweleo (hair). Vijitengo hivi vinapatikana sehemu zote za mwili isipokuwa maeneo ya viganja vya mikono, kwenye nyayo, sehemu za juu za miguu na kwenye midomo. Vitengo hivi hupatikana kwa wingi usoni, shingoni na kifuani.
Tezi za mafuta hutoa sebum ambayo huvisaidia ngozi na vinyweleo kutokuwa vikavu.
Mtu anapokuwa kwenye balehe, tezi hizi za mafuta hupanuka na kuwa kubwa na hutoa sebum (aina ya mafuta) kwa wingi zaidi, hali inayochangiwa na kuongezeka kwa homoni za androgens. Baada ya umri wa miaka 20, utengenezaji wa sebum hupungua.
Sasa mdudu huyo mbona sioni alipoelezewa Mkuu?
🤔Huyo sio mdudu ambae kazi yake ni kula ngozi iliyokufa?
Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app