Huyu ndiye Padri Privatus Mutekanga Karugendo (1956-2021)

Nimeona hapo huyo padre alipotumia toba ya mwenzake kumuangamiza, ni vyema toba ielekezwe kwa Mungu moja kwa moja na sio kwa mtu wa pili aifikishe.
Mwenyezi Mungu hamchukii mwanadamu mpk asimkubalie toba yake moja kwa moja
 
mfumo wa ajabu sana mtu kutubu kwa binadamu mwenzake
huu siyo mfumo wa kiKiristo ni wa kipagani
Mungu ana mgogoro na sisi kwa sababu ya dhambi. Dhambi inaelezewa katika Biblia kuwa uvunjaji wa sheria ya Mungu (1 Yohana 3: 4) na uasi dhidi ya Mungu (Kumbukumbu la Torati 9: 7; Yoshua 1:18). Mungu huchukia dhambi, na dhambi husimama kati yetu na Yeye. "Hakuna hata mmoja aliye mwadilifu!" (Warumi 3:10). Wanadamu wote ni wenye dhambi kwa sababu ya dhambi tuliyorithi kutoka kwa Adamu, pamoja na dhambi tunayofanya kila siku. Adhabu tu ya dhambi hii ni kifo (Warumi 6:23), si kifo cha kimwili tu bali kifo cha milele (Ufunuo 20: 11-15). Adhabu ya haki kwa dhambi ni Jahannamu ya milele
"Maana yuko Mungu mmoja, na pia yuko mmoja anayewapatanisha watu na Mungu, binadamu Kristo Yesu" (1 Timotheo 2: 5).
Huu utaratibu wa kutubu kwa binadamu wenzetu ni kinyume na maandiko ambayo yanasema binadamu wooote, wakiwemo watawa wa madaraja yote( maaskofu,mapadre na papa mwenyewe ni binadamu wa kawaida mbele ya Mungu)
Yesu anawakilisha wale ambao wamemtegemea Yeye mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Anatupatanisha, kama vile wakili anayemtetea mteja wake, akimwambia hakimu, "Hakimu, mteja wangu hana hatia ya mashtaka yote dhidi yake." Hiyo ni kweli kwetu pia. Siku moja tutakuna na Mungu, lakini tutafanya hivyo tukiwa tumekwisha samehewa dhambi kabisa kwa sababu ya kifo cha Yesu kwa niaba yetu. "Mwanasheria mtetezi" alichukua adhabu kwa ajili yetu!
 
Mpango wa Mungu kwenye tendo la ndoa ni:
• Kuleta muungano (union) kwa wanandoa
• Kuendeleza uumbaji (procreation) walioshirikishwa wanandoa
• Kutumia maumbile ya asili

Contraceptives zote zinazoenda kinyume na malengo haya, ikiwemo matumizi ya kondomu, yanaenda kinyume na mpango wa Mungu.

Kanisa Katoliki kamwe haliwezi kwenda kinyume na mpango wa Mungu.
 
Nimeona hapo huyo padre alipotumia toba ya mwenzake kumuangamiza, ni vyema toba ielekezwe kwa Mungu moja kwa moja na sio kwa mtu wa pili aifikishe.
Mwenyezi Mungu hamchukii mwanadamu mpk asimkubalie toba yake moja kwa moja
Kwanza, hatupaswi kuhukumu kwa kusikiliza upande mmoja. Kanisa Katoliki lina sheria na taratibu ambalo kwazo linajiongoza.

Padre (Askofu pia ni padre) anapotoa siri za boksi la maungamo anakuwa ananajisi Saramenti Takatifu ya Kitubio na hivyo anakuwa amejitenga (excommunicated) na Kanisa moja kwa moja bila kujali ushawishi wala nguvu zake na Kanisa humuwajibisha bila kumtazama machoni. Nitakupa mfano.

Mnamo mwaka 1534, mfalme wa Uingereza Henry VIII aliinajisi Sakramenti Takatifu ya ndoa na hivyo akajitenga moja kwa moja na Kanisa. Halikujali nguvu au umaarufu wake kama Mfalme wa taifa kubwa la Uingereza.

Kama Kanisa liliweza kumwajibisha mtu mkubwa kama Mfalme Henry VIII; kwanini lishindwe kwa Askofu Niwemugizi?

Note: Tunaungama moja kwa moja kwa Mungu kupitia Padre. Ni sawa na mtu atoke Dodoma kwenda Dar es Salaam moja kwa moja ila atapitia Morogoro.
 
Kwenye Mathayo 18:18; Yesu amewapa mapadre uwezo wa kufungulia watu dhambi.
 
Je kukiwa na haja ya kibinadamu(afya) kufanya hivo
Mfno kuna wale wanaofanya operation kwa kujifungua not sure but wengi nawasikia wakisema nne mwisho je huyu hana haja ya hizo contraceptive?
Pia kuna wale wanashauriwa pia sababu za kiafya wasibebe pia mimba je hawa wanao hawaruhusiwi
Note: nipo kujifunza
 
Mpango wa Mungu katika tendo la ndoa ni kuleta muungano, kuendeleza uumbaji na kufuata sheria ya maumbile. Contraceptives zote zinazoenda kinyume na hapo zinazuiliwa.

Kwa watu wenye matatizo ya kiafya; Mama Kanisa anashauri na anaruhusu matumizi ya njia ya kalenda ambayo kimsingi haiendi kinyume na mpango wa Mungu kwa tendo hili takatifu.

Ninatumaini nimekujibu vema.
 
Sio kila mtu calendar kwake inaenda sawa, si kila mwanaume au uwezo wa kumaliza nje.
Bado Mungu hamfanyii mwanadamu ugumu kwa kiasi hiko na ndio maana kuna maarifa. Haya maarifa kama yanafaa na yatapunguza athari basi yapaswa yatumike.
Tuishie hapa kwa policy za wakatoliki
 
Njia ya kumwaga nje hairuhusiwi. Njia ya calendar ina ufanisi wa zaidi ya 86%. Usipoifuata ni kwa sababu umeamua kutenda dhambi.
 
Pamoja na hayo, Baba Askofu hakutakiwa kutumia taarifa za maungamo ya Baba Padri kumchukulia hatua! Hii haipo sawa, na nadhani ndio maana wakatoliki "WENGI" hawaungami katika parokia zao!!
 
Nilichojifunza hapa ni kwamba, Askofu Niguwemizi roho yake inaendeshwa na shetani himself and yet anavaa joho la Uaskofu

Pia nimejifunza kwamba Kanisa Katoliki halimtumaini Mungu wa KWELI bali binadamu anayeitwa Papa.

Tatu nimegundua kwamba Kanisa Katoliki hujivika joho la demokrasia nchi mbalimbali wakati ndani ya Kanisa hilo hawaitambui demokrasia

Nne. Hawa watoto wa mapadri tunaoishi nao mitaani hatima yao ipoje kupitia misimamo ya kipagani ya Kanisa?
 
Huo ni uongo mkuu wangu Romans mnaungama kwa Padri sio kwa MUNGU kuwa mkweli
 
Umenena kweli tupu kiongozi wangu ubarikiwe sana [emoji120]
 
Umeuliza maswali magumu sana natamani aje mtu wa MUNGU wa kweli aongezee nyama sio mroma yeyote maana ataharibu radha
 
Na Mungu alipowaambia wana wa Israel wakatubu kwa makuhani, alikuwa analeta mfumo wa ajabu?
Usikosoe anachofanya mwenzio, fanya unachoona kinafaa( kwenye masuala ya imani), maana anafuata maandiko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…