yaani mijitu mingine inapewa sifa bila sababu za msingi, eti huyu naye ni role model bongo. period!
Ndama mbaroni kwa wizi
na Betty Kangonga
JESHI la Polisi nchini linamshikilia mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam, Ndama Shabani (38) au Ndama mtoto wa Ng'ombe kwa tuhuma za kukutwa na gari la wizi.
Pamoja na Ndama, wengine wanaoadaiwa kuhusika na wizi huo ni Sylvester Mashindila (45), Richard Marimi (46), Peter Goyayi (30) au Makoye wakazi wa Mwananyamala kwa Kopa na Charles Mwita (43) mkazi wa Kinondoni.
Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Kamishna Msaidizi wa Polisi na Kamanda wa Kanda Maalum Suleiman Kova alisema watuhumiwa hao walipora gari aina ya Hino lenye namba FDIJKD 11185 maeneo ya Tunduma mkoani Mbeya.
Kova alisema kikosi Maalum cha Kupambana na Wizi wa Magari ya Kanda Maalum ya Dar es Salaam kilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wanaodaiwa kumnywesha dawa za kulevya aliyekuwa dereva wa gari hilo kabla ya kumpora.
Alisema gari hilo lilibeba bidhaa mbalimbali vikiwemo vitanda vinne, magodoro, majokofu, makochi na majiko ya umeme ambapo watuhumiwa hao baada ya kutenda tukio hilo walikimbilia mafichoni jijini Dar es Salaam na kuvihifadhi vitu hivyo Mbezi nyumbani kwa Ndama.
Source: Tanzania Daima
Na ile ya albino sijui iliishaje?