GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Mamia ya wananchi wameshiriki maziko ya aliyekuwa Diwani wa Kamena Halmashauri ya mji wa Geita, Peter Kulwa (67) aliyefariki dunia Juni 13, 2024 na kuacha watoto 34, wajukuu 129 na vitukuu 10.
Kwa mujibu wa risala iliyosomwa na mjukuu wake, Makutano Sadick, diwani huyo alianza kuugua kisukari Mei 2002 na kupatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali nchini na Juni, 2024 akiwa anaendelea na matibabu Hospitali ya Kamanga iliyopo Jijini Mwanza, mauti yalimfika.
Alisema babu yake ameacha watoto 34, wajukuu 129 na vitukuu 10.
Ngoja nami pia sasa nishindane nae kwani mpaka sasa nikiwahesabu Tanzania na Nje wanafikia kama 13 au 15 fulani.