Naandika nikiwa na Masikitiko Makubwa sana Juu ya Taifa langu na Selikali hii ya Awamu ya sita.
Mimi ni Mtumishi wa Mungu nitaandika kwa Kifupi sana.
Mungu alimpa Musa Torati na ndani yake Kulikuwako Sheria Amri na Hukumu, kuwaongoza wama wa Islael.
Amri zake zilikuwa kumi ambazo nimeziona zote zikivunjwa na selikali ya Tanzania, Lakini zaidi naona nyingine zikivunjwa wazi wazi bila hofu wala Uoga.
1. UONGO.
Kila kitu kinachofanywa na hawa watu ni Uongo wa wazi kwa kisingizio cha Propaganda.
Mnawakwaza sana watu hata ambao hawana upande mnawapeleka upande wa haki, Mnajichimbia kaburi kwa Maneno ya Uongo.
2. USIUE.
Hii ni amri ya Mungu inayikataza kufanya Mauaji juu ya Binadamu mwenzio.
Selikali hii imekuwa Ikiua Raia, October 29, Ikiteka, Ikitesa nk
3. WIZI.
Hawa ni Majizi wa kura.
Wanaiba kura kwa kushirikiana na waalimu, polisi na wakurugenzi kuiba matokeo ambayo si halali.
Wanawanyima watanganyika Uhuru wa kuchagua kiongozi wanaye mtaka. Wanawaibia utajili Shahabu, Madini Gas nk
Mungu alikuwa na Makusudio yake vkuviweka hapa Tanzania.
ACHA DHAMBI, ACHA UONGO. MAGUFULI NILIMWAMBIA HIVI HIVI.
MANE MANE TEKELI NA PERESI