Huyo kiumbe anaitwa Sea star au "starfish" kama walivyosema wadau hapo juu. Lakini huyo kiumbe kwa viwango vyoyote vile yeye sio samaki.
Ila kwa sababu ya mazoea, tumezoea kuita viumbe mbalimbali wa majini "samaki". Mifano mingine ni Pweza (octopus), ngisi (squid), kamba miti na kamba koche (prawns and lobsters), nguva (dugong), kasa (sea turtle), chaza (oyster), konokono wagumu na laini (gastropods), kaa (crabs), jongoo bahari (sea cucumber) na wengine wengi.
Kwa ufupi kuhusu huyo sea star.
Kama unakumbuka kuhusu makundi mbalimbali ya wanyama, kama vile ndege, mamalia, amphibia, reptilia n.k.... basi huyo yeye yuko kwenye kundi lake linaitwa "ekainodemata" echinodermata.
Je, ni kina nani hao ?
Echnoderms ni viumbe wasio na uti wa mgongo, wanaopatikana baharini, wenye ngozi yenye miba. Tunaweza "kuwatania" kwa kuwaita "nungunungu bahari".
Ndugu zake sea star katika kundi lao la echnoderms ni sand dollar (kabla ya ugunduzi wa fedha hizi za sasa, hawa viumbe walikua wanatumika kwa ajili ya manunuzi na mauziano), jongoo bahari (holothurians) pamoja na sea urchins (hawa wana miba mirefu kabisa, kama ya nungunungu).
NB: Nimeelezea aspect kibailojia zaidi. Mengine (kama analiwa, ana sumu, maandalizi yake yakoje, n.k wameshaeleza vyema wenzangu hapo juu).