Huyu sio mwizi au jambazi ni Mbunge

Huyu sio mwizi au jambazi ni Mbunge

mng'oa kucha

Senior Member
Joined
Jul 31, 2013
Posts
150
Reaction score
179
Nchi ya Kenya ambayo ni majirani zetu wako katika vuta nikuvute ya uchaguzi baada ya uchaguzi wao kuingia dosari na kufutiliwa mbali na mahakama kuna maandamano yanayo endelea sehemu mbali mbali nchini humo ambapo kama ujuavyo maandamano huambatana na vurugu na wizi.

Kifupi kwa sasa Kenya sio salama kuzuru ambapo nchi tofauti zimeweka travel ban yaani zuio la kusafiri kwenda Kenya kuna watu walikuwa wanasema tuna mengi ya kujifunza kwa uchaguzi unaoendelea Kenya na hali ya kidemokrasia kiukweli sasa hivi siwasikii tena ifuatayo ni picha ya mbunge wa jimbo la embakasi anayejulikana kama Babu owino, hii ni baada ya kukaa rumande kwa muda wa siku 2 kwa tuhuma za uchochezi ambapo alipokuwa jukwaani alisema "kama Gaddafi alitolewa na wananchi, kama Gbgo alitolewa na wananchi na oama Jammeh pia alitolewa na wananchi wewe ni nani wewe ni mtoto wa mbwa"
IMG_20170927_150728.jpg
 
WaAfrika tunataka Demokrasia bila ya kujua Demokrasia ina mipaka na taratibu zake. Demokrasia sio matusi na kejeli katika majukwaa ya Siasa. Babu Owino and the likes ni mfano tosha wa wahuni waliojificha nyuma ya mwamvuli wa Siasa na kuinajisi Demokrasia.
Huwezi kumuita Rais wa nchi Mbwa ukategemea vyombo vya Dola vikuletee "Gift basket"!
 
Mbona wengine huku kwetu wanawaita watanzania wenzao wapumbavu na malofa, wengine wanawaita wapumbavu kabisa lakini hawajachukuliwa hatua yeyote
 
Hawa wapinzani wakenya wanawashwawasha.Yaani wangekuja huku wangekiona cha moto.
 
Mbona wengine huku kwetu wanawaita watanzania wenzao wapumbavu na malofa, wengine wanawaita wapumbavu kabisa lakini hawajachukuliwa hatua yeyote
Rais akikuita lofa au mjinga na wakati no mjinga kweli kwani kuna shida ati wajameni???
 
WaAfrika tunataka Demokrasia bila ya kujua Demokrasia ina mipaka na taratibu zake. Demokrasia sio matusi na kejeli katika majukwaa ya Siasa. Babu Owino and the likes ni mfano tosha wa wahuni waliojificha nyuma ya mwamvuli wa Siasa na kuinajisi Demokrasia.
Huwezi kumuita Rais wa nchi Mbwa ukategemea vyombo vya Dola vikuletee "Gift basket"!
Usikute wewe mwenyewe huwa unawatusi watoto wako "mbwa wewe" na unaona sawa tu,ila akiitwa hivyo huyo unayemuabudu unatokwa povu!! Je angeitwa mtoto wa mbwa wa hapa home!! Si ungekufa kabisa?
 
Mbona wengine huku kwetu wanawaita watanzania wenzao wapumbavu na malofa, wengine wanawaita wapumbavu kabisa lakini hawajachukuliwa hatua yeyote
Inaonyesha hujaenda shule kidogo ndiyo maana hujui maana ya lofa na mpumbavu.
 
Back
Top Bottom