Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Ni muda mrefu nimekuwa nikimsikia akijinasibu kama mchekeshaji maarufu hapa nchini, na kwa kuwa mimi siyo mfuatiliaji wa movie za kibongo pamoja na hao wanaojiita wachekeshaji hata sikuwahi kumfuatilia zaidi ya kupishana naye kwenye kumbi za starehe.
Lakini hivi karibuni nimeona clip moja akimponda Eric Omondi mchekeshaji wa Kenya kwamba hana jipya na kudai Watanzania ni wajinga kumshabikia!
Binafsi mimi siyo na sikuwahi kuwa mshabiki wa Eric Omondi zaidi tu huwa namsikia kwa watu walionizunguka wakisimulia habari zake.
Kauli ya kudai kwamba Watanzania ni Wajinga kwa kumshabikia Eric Omondi ilinishtua kidogo nikalazimika Kumtafuta Eric Omondi kwenye Youtube na Huyu kijana wetu Steve Nyerere.
Ukweli ni kwamba nilichokiona ni sawa na Mbingu na Ardhi, yaani Steve akiwekwa jukwaa moja na Eric hamfikii hata kwa theluthi.
Huyu Mkenya yuko vizuri kwa utafiti na uchekashaji wake unaeliamisha na pia lugha inambeba kiasi kwamba anaweza kwenda hata nje ya nchi kushindana na magwiji wa Comedy kama alivyotoka huyu kijana wa Africa Kusini anayeitwa Noah Trevor.
Ukiangalia vichekesho vya huyu kijana wetu aliyedai Watanzania ni wajinga, anachofanya yeye ni mipasho na si vichekesho kama anavyodai lakini kingine ni lugha ya kiingereza inampiga chenga kwa sababu ya kukimbia shule kwa kutaka umaarufu.
Wasichokijua wasanii wengi hapa nchini hususan comedian ni kwamba ili kujenga soko kimataifa lugha ya kiingereza ni muhimu kwani ndiyo lugha pekee itakayokuwezesha kufika mbali.
Kilichombeba Steve ni Magazeti ya Udaku na yeye kuvimba kichwa na kusahau kwamba elimu ni muhimu kwa fani anayotaka kuifanya. Lakini hajachelewa anaweza kujiunga pale British Council ili kujifunza kiingereza na mbinu mbalimbali za kuzungumza kwenye hadhira.
Hebu tuwaone hawa watu watatu yaani Eric Omondi, Steve Nyerere na huyu Noah Trevor ili muone tofauti ilipo.....