hv sheria za kazi za tanzania zinaruhusu hv?

Master jay

Senior Member
Joined
May 28, 2012
Posts
194
Reaction score
31
mi ni mfanyakazi wa kampuni GFI, kampuni inafanya kazi ya kuweka dawa kwenye mafuta ya diesel na petrol ili yasichakachuliwe, ipo chini ya EWURA, cha ajabu hawa wazungu huwa kila baada ya muda flan hv wanawaleta wazungu wenzao wanawafunga mamitambo flan kwenye mwili wa mfanyakazi mmoja mmoja, wanawauliza maswali huku wanaangalia kwenye laptop, mapigo ya moyo, baadhi ya maswali ni kama, umeshawahi kumwibia mzungu mwenye kampun? Au umeshawahi kuiba kwenye maisha yako? Na maswali mengine kama hayo. Ukishtuka tu mapigo ya moyo yakiongezeka, huna ajira. Maswali ninayojiuliza ni haya {1} je sheria za kazi tanzania zinaruhusu hivi? {2} kwa nin zisiwekwe mahakaman kupunguza mlolongo wa kesi kusikilizwa muda mrefu? {3} afya zetu zipo salama? naomba mnisaidie ushaur
 
Nafikiri swali hili ungejibiwa vizuri kama ungepeleka jukwaa la sheria. Hata hivyo kwa uelewa wangu, hiyo si sawa, kwani ili mfanyakazi aachishwe kazi inabidi kikao cha nidhamu sehemu ya kazi kikae kusikiliza shauri na kumuona ana hatia,mara nyingi vikao hivyo hufanyika mara baada ya uchunguzi kufanyika. Nimepata kusikia kuwa makampuni mengi ya kisasa wanatumia hizo detector za kusema ukweli hata kwenye usaili/interview.
 
Tunaomba jieleze vizuri.
Hao wazungu wenzao nao ni wafanyakazi wa hiyo kampuni?
Je, wasio wazungu hawafungwi hayo mamitambo?
Wenyewe wanasema ni kwa ajili gani hasa?
 
Tunaomba jieleze vizuri.
Hao wazungu wenzao nao ni wafanyakazi wa hiyo kampuni?
Je, wasio wazungu hawafungwi hayo mamitambo?
Wenyewe wanasema ni kwa ajili gani hasa?

hiyo mitambo wanasema ni kwa ajili ya kupima km umeshawahi kuiba, au kushiri. Na wanaopimwa ni watanzania tu, na wanaokuja kutupima ni wazungu. Nafikiri ntakuwa umenielewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…