Master jay
Senior Member
- May 28, 2012
- 194
- 31
mi ni mfanyakazi wa kampuni GFI, kampuni inafanya kazi ya kuweka dawa kwenye mafuta ya diesel na petrol ili yasichakachuliwe, ipo chini ya EWURA, cha ajabu hawa wazungu huwa kila baada ya muda flan hv wanawaleta wazungu wenzao wanawafunga mamitambo flan kwenye mwili wa mfanyakazi mmoja mmoja, wanawauliza maswali huku wanaangalia kwenye laptop, mapigo ya moyo, baadhi ya maswali ni kama, umeshawahi kumwibia mzungu mwenye kampun? Au umeshawahi kuiba kwenye maisha yako? Na maswali mengine kama hayo. Ukishtuka tu mapigo ya moyo yakiongezeka, huna ajira. Maswali ninayojiuliza ni haya {1} je sheria za kazi tanzania zinaruhusu hivi? {2} kwa nin zisiwekwe mahakaman kupunguza mlolongo wa kesi kusikilizwa muda mrefu? {3} afya zetu zipo salama? naomba mnisaidie ushaur