Hydroponic fodder, Mkombozi pekee wa wafugaji wa ng'ombe, kuku, nguruwe, mbuzi na kadhalika

NPK si ni mbolea au ni kitu kingine kabisa? Ngoja nifuatilie hii elimu ya Hydroponics humu then nitakuuliza maswali mengi maana haipo sana kichwani. Lakini kwa kuanza tu, mnasema gharama yake ni ndogo, mfano kg moja ya hiyo mbegu ya shayiri ni sh.ngapi na ng'ombe mmoja kwa siku anaweza kutumia kiasi gani ya hiyo kg? Na mfugo unaweza kumpa hiyo hydroponics tu bila ya chakula kingine?
 
1. KIlo moja ya mtama / ngano ni Tshs 2,000/= kwa hapa Mwanza, na hiyo ni bei ya rejareja. Ina maana ukinunua kwa jumla utakuwa chini.
2. Kuhusu kiasi cha kulisha ng'ombe mmoja binafsi sijafatilia - mi nafuga kuku, kumu mia wanatumia kilo nne za H.Fooder
 
Nashukuru kwa majibu yako. Ila hapo kwenye bei sio kwamba hiyo H. Fodder ndo gharama zaidi nikiwa na maana kama kuku wako 100 wanatumia sh.8000 /day kiasi kwamba hiyo fedha kwa chakula cha kununua isingefika huko. Mimi kuku wangu ni wa kienyeji na nawalisha pumba tu za kawaida hivyo nataka nijifunze hii kitu kama sio gharama sana.
 
Umechanganya ndugu,
kilo nne za H. Fooder sio elfu nane - hiyo ni bei ya mbefu. H. Fooder ni majani pamoja na mizizi na kilo moja ya mbegu ndo inaweza kukupatia kilo 10 za H fooder. Naomba nieleweke kwenye hilo.
 
Ndugu zangu msinione mshamba kwa hili,yan nmesoma post zenu ata nijue hyo H Fooder ni nn kiukwel cjaelewa naona kila mmoja anasifia pia maelezo yanaonyesha faida nyingi kwenye hyo kitu,daah nisaidieni nielewe hyo kitu ni nini na inatumika kwa mifugo aina ipi?
 
Hydroponics Fooder ni nini?
Ni utaratibu wa kuotesha mazao aina ya mtama, ngano, shayiri, ulezi n.k bila kutumia udongo. Ina maana utakachokiotesha kinatumika chote kama chakula kuanzia mizizi hadi majani. Unaotesha kwenye trai na unatumia virutubisho vyenye wingi wa NPK, kwa sasa mimi natumia DI Grow green pamoja na EM na mbegu zinaota vizuri.
Kama wewe ni mfugaji na una shida na uzalishaji wa chakula tuwasiliane ili nikuelekeze.
Trei zipo
Mbegu ziko sokoni
Maji yapo hapo ulipo
Nutrients unaagiza popote
SOP's ndo muhimu na utaelekezwa ...
Uliza jingine
 
Nashukuru sana mkuu kwa maelezo yako pia nmeipenda hyo njia inayotumika,ila mkuu mimi ni mfugaji wa kuku na cfugi wanyama pia kwenye huo ufugaji wenyewe hunipa changamoto ad nashindwa kuelewa faida yake inavyopatikana,vp hyo h food c kwa ajili ya wanyama pekee au ata kwa hawa ndege?
 
Kuku wakipatiwa hiyo chakula wanakula sana tena sana. Inasaidia kwa sababu huangaiki tena kuwatafutia majani.
 
Haya ndo mambo vijana tunatakiwa kushirikishana, sio ya kijingajinga na ndoto za alinacha. Mkuu hongera sana, na utabarikiwa sana. Binafsi ntaangalia uwezekano wa kukuona, niko Simiyu. Na ukame, uhaba wa maeneo ya malisho ni shida sana kwa wafugaji wetu.

Naamini nikielimika ktk hili ntawaokoa wengi sana. Kwanza nitajaribu kuwashirikisha wataalamu wa huku, tukishindwa nitakufuata Mkuu.

Nadhani huu utamaduni ukiendelezwa wa kushirikishana tutafika mbali sana, Tanzania yetu iko mikononi mwetu Mkuu.
 
WE ANDAA TREI, MBEGU NA NUTRIENTS
 
Shukran sana kiongozi
 
Mkuu hii booster ya majani unachanganya na chakula cha kuku au?

Shukran
 
Kiukweli ukikutana na mtaalam wala hautatumia muda mwingi kuelewa kinachoendelea. Mimi atakayehitaji maelezo namkaribisha - tena hatua kwa hatua. Kikubwa ni kuandaa muda wa kupeana maelekezo. Ukifanikiwa wewe unakuwa umesaidia jamii.
Mkuu unapatikana wapi na unaweza kunisaidiaje step by step?

Ikiwezekana nije kwajili ya shamba darasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…