Hydroponic fodder, Mkombozi pekee wa wafugaji wa ng'ombe, kuku, nguruwe, mbuzi na kadhalika

Haya ma Hydroponic fodder ni sawana sungura,Kenyawafugaji wotewakubwa wa Kuku, Ng'ombe hakuna anaye tumia hii kitu, wanao itumia niwale wana uza, yaani anakuwa na kukuwake 6 wa kuzugia kuwalisha fodder au Ng'ombe wake mmoja, ila kiuhalisia hikitu haina tija
 
ina tija sana tena sana - we hujajua tu. faida ya kufuga inapungua kutokana na gharama za kulisha kuwa kubwa.

Jambo jingine, wale ng'ombe walokufa karagwe kwa kukosa chakula wasingekufa kama wafugaji wangekuwa wkijua hii njia ya uzalishaji wa chakula hiki.
 



Mm nlipewa hii formula
Chakula hicho ni kwa ajili ya kuku, ndani yake hakuna majani .. na hiyo ni shida sana kwa kuku wetu.

Chakula hiki huwezi kumulisha mbuzi wala nguruwe wala ng'ombe

Hydroponics ni chakula kwa ajili ya mifugo yote, sungura, kuku, ng'ombe, mbuzi, kondoo, bata n.k

Mfugaji wa ng'ombe anayetumia chakula hiki ana uhakika wa kupata maziwa zaidi ya lita 10, hii ni 0 grazing - mifugo haichoki.
 
Kilimo cha hyroponic fodder katika picha, inaelekea watu wengi hawajaelewa hii aina mpya ya kilimo cha kuotesha majani kwa ajili ya kulishia mifugo.



Ni kilimo cha kuotesha majani kwa kutumia nafaka zenye virutubisho vingi hasa shairi, ngano, mtama, mahindi
Angalia huyu mkulima katika picha hapo juu. Ametayarisha mbegu zake kwenye try, angalia try za juu zipo tayari kulishia wanyama, inachukua siku sita au saba tangu mbengu zinapomwagwa kwenye try



Chakula cha mifugo kipo tayari mkulima anakiondoa kwenye try tayari kulishia wanyama.


Mkulima analisha ng'ombe


Kuku nao wanafurahia chakula chao.
 
Kama
Kama jina lako!

Ahsante ... nimefurahi sana,

Picha inabeba ujumbe mzito sana zaidi ya maneno. Naamini wale ambao wako tayari kuwasaidia wafugaji waeneze maarifa haya.
 
Kwa wale mliopo sumbawanga mni_pm niwafundishe.... Naijua vizuri.. Karibuni.
 
Huu utaalamu mzuri sana.
Kiukweli ukikutana na mtaalam wala hautatumia muda mwingi kuelewa kinachoendelea. Mimi atakayehitaji maelezo namkaribisha - tena hatua kwa hatua. Kikubwa ni kuandaa muda wa kupeana maelekezo. Ukifanikiwa wewe unakuwa umesaidia jamii.



Booster unachanganya na maji unayomwagilia.

Kwa wale mliopo sumbawanga mni_pm niwafundishe.... Naijua vizuri.. Karibuni.
 
hongera mtoa uzi, naona mapinduzi yanaendelea! hv ndege mmoja hasa kuku anastahili kula kiasi gani cha hiyo fodder kwa siku nzima? nahitaji makadirio tafadhali...
 
Mkuu, "SOP" ndio nini. ?Naomba msaada hapo..
 
hongera mtoa uzi, naona mapinduzi yanaendelea! hv ndege mmoja hasa kuku anastahili kula kiasi gani cha hiyo fodder kwa siku nzima? nahitaji makadirio tafadhali...
Gram 80 tu, kwani msosi wake kamili ni gm 125 tu kwa siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…