Mzuzu,
Maswali/swali lako halieleweki vizuri.
Unauliza - "hivi mtu akikutumia I-20 ya shule ana uwezo wa kuifuta ukiwa tayari umepata Visa?"
Jibu - Nita-assume unaposema "mtu" unamaanisha "chuo" kwa sababu I-20 ni document inayotoka kwenye chuo ulicho-apply na sio kutoka kwa mtu binafsi. Sasa basi, jibu ni ndio, chuo kinaweza ku-cancel I-20 iliyo issue hata baada ya kupata Visa.
Kuna sababu mbalimbali chuo kinaweza kuhahirisha I-20, lakini pengine sababu mzito ni kama chuo itabaini kuwa ulitumia document au information feki kwenye application.
Kwa hiyo, once chuo kiki-cancel I-20, student Visa yako uliyoipata inakuwa inactive.
Unauliza - "ukiingia US na student VISA bila authorization to travel letter hautaruhusiwa kuingia states?"
Jibu - unaposema " bila authorization to travel letter" unamaanisha bila I-20? Kama unamaanisha bila I-20, jibu ni ndio hautaruhusiwa kuingia States. Ukija U.S. kama mwanafunzi, utakapowasili kwenye Port of Entry (Airport ya kwanza utakayotua ndani ya anga la U.S.), utatakiwa kuonyesha documents mbili muhimu - Paspoti yako yenye visa halali na I-20 yako inayoonyesha shule unayokwenda. Sasa kama hautakuwa na I-20, basi hautaruhusiwa kuingia U.S. hata kama una visa halali.
Au
Unaposema "authorization to travel letter" unamaanisha barua gani na kutoka kwa nani?