MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
tuna lugha ambayo imetuunganisha pamoja na kuweka tofauti zetu mbali,tanzania ni nchi ambayo unaweza kuishi na mtu zaidi ya miaka bila kujua kuwa huyo mtu ni kabila gani na kwa nini uongee lugha ya kabila lako katika mazungumzo ya watu watatu kisa yupo mmoja wao anaekuelewa ijapokuw ipo lugha uwezayo kuongea na kila mtu akakuelewa hivyo basi lugha za hasili kwa Tanzania huzungumzwa katika mkusanyiko wa watu wanayoifahamu tu!
Sent using Jamii Forums mobile app
Hamnaa, nyie watumwa mumefungiwa ndani ya lugha moja tu, wengi wenu hamna uwezo wa kuongea zaidi ya Kiswahili halafu mnapenda sana kujitetea eti kisa kinawaunganisha ndio mumezembea kujifunza lugha zingine. Sayansi imebaini kwamba mtu mwenye uwezo wa kuongea lugha kadhaa huwa anaboresha hata kasi yake ya kuelewa mambo, sio unakaa kama mbumbumbu lilifungwa kwenye lugha moja.
Nyie mtu akiongea lugha ya asili mnamuita mshamba, akijifunza kingereza au lugha yoyote ya kimataifa mnamuita mtumwa, mna tabia za kuwaburuta wenzenu ambao wanajaribu kutanua uwezo wao wa lugha.
Sisi hapa Kiswahili kinatuunganisha kama taifa, tunakipenda sana, lakini pia tunaenzi lugha zetu za asili za mababu zetu, hatuwezi kuacha asili yetu, na pia tunajifunza na kuongea lugha za kimataifa na ndio maana mnaona tunatawala ukanda wote huu kiushawishi, kiuchumi, kielimu, kijeshi na kwa kila kitu.