I am depressed. Naombeni ushauri

Pole, itabidi umpeleke kwa mwamposa akaombewe C's inaonekana anakaujinga flani hivi.
 
Dj nipigie nyimbo ya mume bwege🤣
 
Pole!
Umesema ni last born sio!!?bhas ana akili za kivulana sana,natamani nimpige kofi!
Kuhusu kujenga Hana msukumo coz halipi Kodi na nyumba ni ya mama yake kifupi uliolewa na mtoto wa Mama!

Simama mwenyewe after all nyumba ni ya mama na watoto wake wanaume tuliowengi inaonekana makaburi ndio nyumba za kudumu!Hufa mapema na kuwaacha nyie mki enjoy na kumiliki!!

Ingia mzigoni mwenyewe na usimshirikishe sana muache anunue chakula TU na mahitaji mengine basics!!

Kuhusu shule nadhani anaona elim ni Bure na haina ajira kwahiyo ni kama anaona atajichosha you kwa kulipa ada halafu aki graduate kijana atakuja kulelewa TU nyumbani,

Unaweza mpeleka mwanao kwenye shule za kati huku ukitafuta kiwanja na kujenga pole pole!

Kwa changamoto nyingine unaweza no pm!
 
Haya mambo mengi mlitakiwa kuzungumza na kupanga kabla ya ndoa na mtoto.

Hili liwe somo kwa wanaotaka ndoa.
 
Wanawake kiafrika mnaubinafsi Sana .


Kama anapata 800K na wewe unapata 2.+M inakuaje unamwambia awe omba omba .

Kwanini usinunue uwanja na usimpe mtaji.
 
Pole dada mkubwa Sasa kimsingi mimi Sina ushauri mkubwa zaidi ya kukwambia
👉 (tafadhali hizo ni dharau Yani mwanaume Ana mshahara afu akakope kwa ndugu yake? Haiji akilini bank zipo mwambie shemeji yetu akakope huko kwenye taasisi kukopa na watu ni kutafuta lawama baadae
👉Usije ukaomba ushauri kwa marafiki zako au marafiki ama ndugu mbaya/adui muharibifu wa mahusiano huwa hatoki mbali
👉Biashara si kwa ajili ya Kila mtu (huyo mwenzio Hana entrepreneur spirit)
Sasa basi (kuwa na kifua hayo ni mambo madogo sister mkubwa)
Am done
 
Duh pole
Kuhusu shule mwambie atafute anayoweza afford...
Kuhusu maendeleo fanya unayoyaweza mengine muachie afanye
Punguza kufanya majukumu yake
Atabweteka huyo
Nunua kiwanja andika jina lako na la mtoto
Anza kujenga mdogo mdogo
Akija kustuka umefika mbali
 
Haya mambo mengi mlitakiwa kuzungumza na kupanga kabla ya ndoa na mtoto.

Hili liwe somo kwa wanaotaka ndoa.
Kibongo bongo hili ni gumu sana ~ kupanga kabla ya kuoana huku kwetu ni jambo ambalo limekaa mbali mno na upeo wetu wa kufikiri
 
Una mshahara wa 2.3 m, yeye ana mshahara wa laki 8.

Umefungua biashara yako bado changa.

Umempeleka mtoto shule ya gharama ila wewe utachangia usafiri na uniform.

Umempa wazo afungue biashara ila mtaji akaazime kwao.

Ushauri wangu mpende mume wako kwani mpo pamoja ila sio wamoja.
 
We
We ni mama Bora kabisa.
 
Nimeshaona last born wanaojitambua na wanafanya mambo makubwa tu.

Hali kadhalika nimeshuhudia firstborn wakishindwa kufanya mambo yao ya kimaendeleo.

Kutoa ushauri hapa inakua ngumu kidogo, hua ni vizuri kusikiliza pande zote mbili ili kupata hali halisi ilivyo.

Kwa haya maelezo uliyoyatoa na Kwa uchache sana, baba watoto amekata tamaa na Ile hali ya kupata kila kitu bila kujishughulisha imemuathiri mno saikolojia yake.

Hachukulii maisha Kwa mtizamo wako na ndio maana mtapishana sana kwenye Kila jambo mnalopanga

Sasa hapo wewe ndio wa kumsaidia ili muweze kujikwamua hapo malipo. Ukipata depression ndio mbaizika familia.

Huyo jamaa self esteem Iko chini sana, na Hilo ndio inabidi lifanyiwe kazi. Bila kutambua nafasi yake, hawezi kupambana ipasavyo na hatachukulia maisha Kwa uzito na mzigo ulionao.
 
Chakukushauri fanya kile unachoweza kwa maendeleo yenu huku ukimshirikosha. Swala la shule ya mtoto mbona zipo shule za bei ya kawaida na zinafanya vizuri tena ada na usafiri unalipa kwa term nne bila shida?
Wazo zuri hili
 
Kwanza ilo jambo la kawaida sana sioni sababu ya wewe kupata depression, pili tafuta shule ya bei ndogo mumpeleke mtoto wenu vya bei ya juu viacheni, tatu uyo mme wako anaonekana hana wivu na maendeleo kingine yawezekana anajivunia ni mtoto wa mwisho anajua nyumba ya urithi ipo ambayo munayokaa hapo ivyo ndio sababu hajitumi
 
Kwa ujumla nyinyi KIPATO chenu Cha familia ni laki 8 ishini humo.
Bajeti zenu mnazopanga kuanzia chakula, mavazi na shule pigieni hesabu ya laki 8.
Biashara anaweza kufanya na ikafa pia maana sio uhakika Kama itaongeza KIPATO.
 
Nafikiri issue yaweza kuwa beyond mtaji maana hata ukipatikana mbona kama mfanyabiashara hayupo?
Hapa ishu bwana last born aamke...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…