Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Tulikuwa tumetoka outing kwa ajili ya kupata winywaji na kubadilishana uzoefu, na katika mazungmzo yetu tulifikia mahali tukajikuta tukizungumzia masuala ya familia na hapo ndipo aliponijulisha kwamba aliachana na mkewe miaka miwili iliyopita nchini Uingereza baada ya kuishi pamoja kwa miaka mitano na kujaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume.
Huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni mfanyakazi mwenzangu ambaye ndio amejiunga na Kampuni yetu akitokea nchini Uingereza.
Alidai kwamba mkewe alikuwa ni kero kero kero, na mtu ambaye yuko juu kwa kila kitu, kwa kipindi cha hiyo miaka mitano, alichoishi naye alikjikuta akiwa kama yuko Jehanamu. Kwani hakuwahi kuifurahia ndoa yake kamwe tangu walipojaaliwa kupata huyo mtoto wao pekee.
Aliniambia kwamba alijitahidi kuilinda ndoa yake na mkewe lakini ilifika mahali akajikuta kama anafanya kazi bure, huyo mkewe hakuonekana kujali wala kuonesha ushirikiano na ndipo alipofika mahali akaamua bora yeshe…………………..Wakayamaliza kisheria na sasa anayo furaha kuachana na mkewe na wala hajuitii kitendo hicho.
Sikutaka kuchangia chochote wala kutoa maoni yangu, bali nilimpa pole na nikabadilisha topic maana niliona anataka kuchakachua outing yetu.
Hivi inakuwaje, haya mambo jamani……………………….Watu leo wanaoana wakiwa na furaha na amani, lakini mara tu, watu wanaachana baada ya sarakasi nyingi na kufikia kutamka maneno kama haya……!