I am looking for a business partner in an attractive Agro-processing business located in Dar

Ni sawa kabisa watanzania tujifunze partnership ndo maana hatuendelei tunaishia kukopa kwa riba kubwa kwa vibiashara vidogo tusivyokuwa na uzoefu. Hapa kama mtu hana idea hana muda sana wa kusimamia biashara na pia hana capital kubwa ni vizuri ukaweka hapa ukijifunza baada ya muda ukahama au mkatanuka na kila mtu akasimamia branch Fulani kwa jina lile au kubadili lakini kwa kutumia ujuzi aliopata hapa.
 
Ni sawa lakini inabidi uwe wazi startup capital ni kiasi gani, equity pia partner anatakiwa kuchangia kiasi gani ili business ianze location bila kutaja wilaya walau mkoa ili kwa kusoma tu hapa mtu aweze vutiwa kuku pm,
 
Watu wengi wenye elimu na vipaji vya biashara wenye fire ya kufanya biashara na kufanikiwa, wanahangaika kutafuta mitaji ya biashara wanakosa. Ila mtu ka wewe ambaye uko katika nafasi nzuri ya kupata mtaji kutoka benki na kuanza kufanya biashara, unakaa kupoteza myda kutafuta partners, ambao ni ngumu kupata. Hii yote ni sababu au cover ya uoga, hofu na self doubt uliyonayo kuhusu ufanyaji wako wa biashara. Kama ungekuwa unajiamini sidhani hata kama ungekuwa unapoteza muda wako humu.
 

Ngoja niongezee tu kidogo ulichosema kinaweza kuwa na ukweli kabisa kwamba hana uhakika na biashara yake. Lakini hata kama ni mimi nakuja kuwekeza kwake lazima nijue security ya investment yangu, je! hii business ina assets zipi ambazo zinaweza kuwa guarantee ya investment yangu. Na lazima hii partnership itafanywa kwa kisheria na mashahidi. Kwahilo anakuwa hajaepuka kupoteza mali iwapo business haitakwenda kama ilivyo kwenye makubaliano.

Lakini pia muelewe tofauti ya kutafuta financial investment kupitia bank na business partner . Bank wanakupa hela na wanaweza kukusaidia kwenye general advice za kuendesha biashara. Baada ya hapo unabeba mzigo wako mwenyewe. Lakini kwenye business partner anakuja na zaidi ya financial investment kama vile experience, networking, ideas, knowledge n.k. Hivyo basi kwa mimi huwa naona business partner ni better than a bank kama hauna mtaji wa kutosha sababu kuna zaidi ya pesa unapata kutoka kwa business partner.
 

Mkuu tutake radhi mbona unatudhihaki, huyu jamaa anatafuta business partner na ukielewa tofauti ya bank na business partner usingesema hayo uliyoyasema. Kwa taarifa yako kupitia huu mtandao umewawezesha watu kuwekeza kwenye biashara ikiwepo mimi mwenyewe. Sasa ukisema anapoteza muda unakuwa hujamtendea haki na wala hujawatendea haki members.

 
Mkuu! nimekuPM tazama inbox yako halafu lete habari. Ahsante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…