I dont understand this

I dont understand this

nameless girl

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2012
Posts
4,195
Reaction score
2,678
Endapo mtu akapewa adhabu ya death punishment, je anaweza kutumia katiba ya Jamhuri ya Muungano kujitetea kwani hairuhusu mtu kuuawa na kwanini sheria hizi zipingane wakati zinatumika mahala pamoja (penal code na constitution)?
 
Yaah kila mtu ana haki ya kuishi lakini ina potokea umevunja sheria ni kujinyima haki yako wewe mwenyewe wala si sheria!

Kama kosa ulilofanya lina adhabu hiyo au lina stahili adhabu hiyo basi sheria itafata mkondo.

Hivi una jua kila mtu ana haki ya kuwa huru lakini kuna watu wana jinyima uhuru wenyewe kwa kufanya makosa! Hivyo basi tupo huru na tuna haki ya kuishi bila kuvunja sheria:

Tunapo enda kinyume na sheria tumejinyima haki zetu wenyewe hivyo vifungu vingine kutuhukumu.

United republic of tanzania 1977, haki ya kuishi
 
tafuta kesi ya R v. Dominick Mbushuu ile ya CAT imeelezewa ila unaweza kuanza na ile ya High Court ya Mwalusanya
 
Ni kweli Ibara ya 14 ya Katiba inasema kuwa "Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria."

Lakini Ibara ya 30(2) ya Katiba hiyo hiyo inasema kuwa "Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia
sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa mujibu wa sheria hiyo..."

Kwa maana nyingine, Katiba inakupa haki yako kwa mkono wa kulia halafu inaichukua haki hiyo hiyo kwa mkono wa kushoto.

Ndiyo maana unakuta vifungu vingi tuu kwenye Katiba vinaanza kwa kusema "Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria iliyotungwa na Bunge, blah bla blah. Penal code imetingwa na bunge na haitakiwa kuadhiriwa na vifungu vya Katiba.
 
Back
Top Bottom