Ni kweli Ibara ya 14 ya Katiba inasema kuwa "Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria."
Lakini Ibara ya 30(2) ya Katiba hiyo hiyo inasema kuwa "Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia
sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa mujibu wa sheria hiyo..."
Kwa maana nyingine, Katiba inakupa haki yako kwa mkono wa kulia halafu inaichukua haki hiyo hiyo kwa mkono wa kushoto.
Ndiyo maana unakuta vifungu vingi tuu kwenye Katiba vinaanza kwa kusema "Bila ya kuathiri Katiba hii, au sheria iliyotungwa na Bunge, blah bla blah. Penal code imetingwa na bunge na haitakiwa kuadhiriwa na vifungu vya Katiba.