I feel like I want to die

Mkuu, tena ni bora hata wewe umeishia kidato cha sita. Kikubwa muombe Mungu akujalie pumzi na uendelee kutafuta (mtafutaji hachoki, akichoka ameshapata) maana maisha haya si ya kujikatia tamaa. Nenda hata kwenye makanisa ya dini tofauti tofauti nadhani huwezi kukosa msaada, jitume na acha kufikiria kulaumu kwanini baba yako hakukuwekea hazina ila kaa ukijua bila jasho lako ni ngumu mkono kwenda kinywani.
Pole sana Mkuu.
 
Hii inanionesha ni kivipi dunia ilivyo...
Sikushauri ujiuwe

naona kama duniani kuna siri ambayo hatujaigundua lkn huenda mbeleni tukaigundua.
lawama anazopewa sizani kama yy ndo anahusika kwa hili na mengine.. naona kificho kimejificha kwake but chanzo kipo nyuma yake..!!

sikushauri ujiuwe....
 
Pole Sana kijana. Jamani wadau acheni kumbeza kijana WA watu. Nadhani Yuko idle ndo maana anapata hayo mawazo. Pengine hujui amepitia mangapi mpaka kufikia kulialia huku jf na kutaka kujiua, wengi wanapitia magumu ILA yanatofautiana Sana na PIA tunatofautiana uvumilivu na kiwango Cha kuyabeba matatuzo. Mi nionavyo Ni kwamba mleta mada Ana stress na amechanganyikiwa anatakiwa apate watu WA karibu awaambie kwa ukaribu yaliyomsibu hadi kuamua kuwaza kujiua.. Nadhani akili yake ikikaa sawa ataona kuwa alikuwa anafanya vibaya ILA kwa sasa msimkashfu sababu waliopitia hayo wanajua akili inakuaje na kwa kijana mdogo kama huyu Ni rahisi Sana kuchanganyikiwa
 
Shukuru Mungu mwambie asante kwa maana una macho una mikono una miguu jiamini amka pambana sali acha mawazo potofu
 
BADO HUJAFA TU NASUBILIA MLEJESHO.

SWISSME
 
Sidhani kama jibu lako Ni sahihi Mkuu.. Watu wanatofautiana Moyo WA uvumilivu na hii inatokana na malezi na mazingira alokulia. Hajasema Ni matatizo gani amepitia hadi kuwaza kujiua. Mi sidhani kama la kukosa mahala pa kukaa au kufukuzwa Ni tatizo lilomfanya ajiue ispokua napata hisia kua Kuna mambo mengi amepitia hadi kufikia kuwaza kujiua. Nadhani alikosa WA kumwambia haya that's why akaja kusemea huku. Unajua mtu akificha kitu rohoni Ni vibaya zaidi ILA ukiongea linalokusibu huku jf unapata kidgo amani ya moyo. Nakwambia Ni bora alivokuja hata kuandika hapa na wazo Hilo litakosa nguvu na hatopata wazo la kujiua tena lakin angekaa nalo moyoni hakika angejiua kbla hata ya usiku huu
 
Samahani wewe ni Ke au Me ?? Kuna mwanamke namjua yeye ni yatima ,mapito aliyo pitia kwenye hii dunia ilifika mahali nikaacha kuamini kama kweli Mungu yupo ,Siwezi kusema aliyo yapitia ila bora hata wewe una mama yako mzazi japo sijui uhusiano wako na yeye ukoje na walau umesoma kuna mtu hajui hata shule ni nini ,kuna watoto wa mitaani wamezaliwa wakatupwa kwenye majalala wamekua maisha yao hawajui wazazi wao ,kuna vilema wanazaliwa hawana Miguu,macho nk na wanaishi seuze wewe unaona,unatembea ,una akili timamu , .....hakuna chenye mwanzo kisichokua na mwisho na kujiua sio ndio njia ya kutatua tatizo ,
NB badilisha hilo jina la POINT OF NO RETURN ,WEKA WRONG TURN huenda ukashtuka na kuona unachotaka kufanya sio sahihi
 
Wanaotaka kujiua hawasemagi mdogo wangu,wanasemaga kwa ujumbe ambao huacha maswali mengi.
Acha huo upumbavu wa kutaka kujiua kwanza jamhuri hii ya magufuli yaweza kukushitaki kwa kutaka kujitoa uhai.

Shida wewe unania makuu umejaribu hata kwenda kwenye maghorofa yanayojengwa kuwa foreman umeshindwa?
Umeshindwa kuomba kuwa saidia fundi kwenye sites za ujenzi kwa siku elfu 10?
Kuna watu wana hizo form 6 zao,degree na masters nao hawana kazi kwa hiyo wajiue.
Kwa hiyo unadhani kufa ni kupumzika?
Hayo unayopitia ukija kufanikiwa kwenye maisha ndiyo yakakayokuimarisha hata ukiitwa kwenye interview watu watapenda kukusikiliza kwani utakuwa na ushuhuda halisi
Mwanaume hajiui kirahisi hivyo,amka pambana usiwaze kujiua wakati tanzania bado ina maeneo ya kilimo.
Acha kabisa mawazo yako hayo ya kipuuzi na kipumbavu je ungekuwa na je mbona hao wanaokutana na panga la magufuli hawajinyongi wanakomaa kiume sembuse wewe.
Ukiona huu ushauri wetu ni ujinga basi amua lolote lakini wengine tukiweka misala tuliyopitia wewe ni cha mtoto sana.
Yaani umeshindwa hata kuwa dancer wa tigo kwenye promotion za 4G sim card acha bwana hizo,usipende makuu kijana elimu ya form 6 bado sana una maisha bado
 
haaahaahaa mwenye nia kweli ya kujiua hawezi kuandika hilo gazeti hapo juu na kulitundika huku JF...wewe huna tofauti na kina wema sepetunga,kajala, aunt Ezekiel et al, unatafuta kick tu hapa jukwaani.
 
Halafu mpenzi wako unamuachaje umemuaga?
Yaani unataka kumwacha kweli
 
Pambana pambana pambana aisee...
Mfano mzuri baba yangu mzazi mama yake alifariki akiwa na miaka nane...ameishi kwa kutapa tapa vibarua visivyoeleweka mpaka Mungu kamshika mkono leo. Unafundishwa kuwa mwalimu bora baadae kwa wenye shida kama zako ndugu. Angekata tamaa angekuwa wapi ? Fight fight fight....kama huna akili tumia nguvu....ili mradi usiende kinyume na mapenzi ya Mungu...penye ugumu ndio neema hukaribia. Ukijiua tu ndio mwanzo wa jehanamu...utatamani urudi huku...na hutakuwa na nafasi tena. Pambana ! Pia tafuta mahali utakapo kuwa unamfanyia Mungu ibada.
 

ramosa mtoto wa kiume kuwa that fragile sio kabisa na katu siwezi kuanza kumuonea huruma kwasababu tuliopitia magumu ni wengine mno. Kama wote tungelialia badala ya kupambana na maisha basi nadhani sehemu kubwa ya dunia ingekaliwa na watu wasiojishughulisha, kazi ingekuwa kupokezana kulia tu.

Kitu kingine, rudi usome thread yake upya utaona kwamba analalamika sana kuhusu kutokuachiwa urithi, kufukuzwa, kuambiwa awe gay baada ya kumlilia mtu shida na kuwa na sehemu ya kukaa kwa muda wa siku 5 tu zijazo. Kiini cha tatizo lake ni HELA. We mwambie unampa mil. Moja tu sasa hivi uone kama hatosema shetani alikuwa akimshawishi kujiua japo yeye anapenda kuishi. Kama mtoto wa kiume he has to toughen up. Kwani haoni vijana wengine wanavyohangaika kutwa juani kutengeneza matofali, kubeba zege, kuuza karanga, maji na vitu vingine vidogo vidogo bila kumlalamikia yeyote? Ye anakaa mahali na smart phone yake (hata kama ni ya mchina haipungui 50 000) na bundle ananunua kisha anaanza kulalamika mtandaoni. What good will that do?

Alichotakiwa kufanya ni kuja na kuomba ushauri /muongozo wa biashara ama shughuli gani afanye ikiwa ana hela kidogo tu. Yani kama yuko Dar, njaa atakufa kwa kupenda na sio kulazimika maana hapa mjini mtu akiwa tayari kuhangaika na kujituma sh. 5000 tu ni mtaji ambao unaweza ukampa faida ya 2000-kuendelea mbele,kila siku.
 
mbona sioni akijibu comments za wakuu hapa!!!? au ndo keshatangulia mbele za haki!?

anyway..kama bado upo nakushauri ukifika muda wa kujiua, usijiue kwa huyo masamaria mwema aliyekuweka kwake kwa siku tano...utamwachia shida huku nyuma bure..
wasalaam waliotangulia
 
Dogo,, hilo wazo sio lako, pole sana kwa unapopitia najua ni ngumu sana wengi kukulewa lkn tazama kuwa Mungu ana makusudi na wewe na ndio maana mpk sasa hujafanikisha mpango ambao shetani anao juu yako, husijue nitakutafuta siku siku si nyingi na mambo yako yatabadilika nitumie number yako
 
I can not say a thing, i can not help, im just crying, please come back and say this is just a story, please !!!
My assumption is that this is a story. Why? The guy with such degree of problems has a cell phone or computer access to write a thread on JF web!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…