I Hate Swahili Because It Is Purely Arabic

I Hate Swahili Because It Is Purely Arabic

Status
Not open for further replies.
Kiingereza nacho hukijui vizuri vinginevyo usingeandika ' It is purely Arabic'.

Tafuta maana ya neno pure katika kamusi ubaini uwongo wa heading ya thread yako.
 
Dear MOD,
As a custom I would start by the famous mantra ''Naomba Muongozo wako''.
1. I wonder if the post (by Jerusalem) is in the right forum.
2. Do the contents make sense to you and your audience?
3. Does this kind of post presents the values of your respected website!
4. Does this make the writer and a reader honor your motto ''Home of great thinkers''?
5. For how long we gonna tolerate this kind of insanity at the cost of our nation
6. Is it not true that we need to co-exist regardless of our differences, so that together we can forge the national agenda as one people?

Dear MOD, I wonder if there is any criteria used to ban the offenders of the forum in any way. Otherwise this kind of profanity would have not been allowed with impunity. The impact of hatred will be felt by entire society including the political parties. I will assure you that , there opportunistics who are quick to concoct what we read in your website and certain political party. Apparently you may think it is some individuals who are traumatized by the blasphemy from this malicious element, however I can categorically say, the same does harm than benefit to vast majority, the time will tell us all.
I am entitled to my opinion and not fact, therefore I hope my statements will not affect your modus operandi rather improve the image of the forum. I always stand for what I believe is right!

Thanks
 
Kwa hakika maradhi ya akili yanawapata watu wengi ktk nyakati tofauti, na dalili zake zipo za namna nyingi zisizo na ulazima wa kufanana baina ya mgonjwa wa kwanza hadi mwingine, ingaa tabia ya kuchukia kibubusa kisicho stahili kuchukiwa huwa ni dalili inayo wapata wengi, tatizo lake kubwa ni moja tu hadi pale wenye akili timamu kiasi wanapo anza kufikiria kuwa huenda hizo zikawa ni dalili za ukichaa huwa tayaari ni very very too late.

Yuko bwana mmoja alianza kwa kuuchukia muda wa saa saba mchana na hasa ya Dar es Salaam tena ya nyakati wa jua kali, eti kwa sababu kwanza inaitwa adhuhuri, pili inamletea joto kali kiasi anashindwa kukutana na "mwenzia wake" muda huo na tatu kinamuonesha kivuli chake kuwa ni mfupi sana kuliko uhalisi wake. Badae akaja kuupenda sana muda wa la siri kwa sababu kuna neno "la siri" limetumika katika kuutamka kwake na pia anapovua nguo hujiona kwa njia ya kivuli kuwa ana kiungo kirefu kupita punda

Najitahidi kuinamisha kichwa isije ikawa tayari nimeshachelewa katika kupata jibu la kwa jambo lipi liliokufanyia uisilamu hadi uuchukie kiasi hicho au kwa jema gani uliyokufanyia ukristo hadi uupende hivyo.

Kuna haja ya kutongoja dalili zitokee ndipo tutibu bali tucheki afya zetu za akili hata kila tunapotaka kuamua kukipenda au kuchukia chochote.
 
Nimebambika vi-major na hili jibu!

AWAU'ZA WASWAHILI

1

Risala enuka hima, sikae 'kataghafali
N'na jambo 'takutuma, ubalegheshe suali
Nipate jawabu njema, yenye amani na kweli
Nauliza Kiswahili, ni lugha ya watu gani?


2
Lugha nyingi duniyani, zatamkwa mbalimbali
Na zote ulimwenguni, zina wenyewe mahali
Si Hindi Si Uzunguni, mewaumbia Jalali
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani ?


3
Wakamba wana kikwao, lugha yao ya asili
Na Wazungu piya nao, wana zao mbalimbali
Na Wameru wana yao, wengine ni Wasomali
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani ?


4
Wahindi wana Kihindi, kwa kabila mbalimbali
Na Wanandi ni Kinandi, ndizo zao akuwali
Wengine ni Wakilindi, wana yao ya asili
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani?


5
Kuuliza Si ujinga, musinifanye jahili
Nautafuta niuwanga, tuzinduwane akili
Ndipo shairi hatunga, kubaleghesha suali
Nielezwe Kiswahili, ni lugha ya watu gani?


6
Mara nyingi husikiya, kuwa hichi Kiswahili
Hakina mtu mmoya, ambaye ni chake kweli
Na wengine huteteya, kina wenyewe asili
Ndipo ha'mba Kiswahili, ni lugha ya watu gani?



7
Masai ana kikwao, lugha ya tangu azali
Na Mahara wana yao, wengine Mashelisheli
Na Waluo lugha zao, Si sawa na Maragoli
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

8
Na jamii wengineo, wana lugha mbalimbali
Na kujuwa ya wenzao, ni kujifunza ya pili
Lakini wana na zao, lugha za tangu asili
Jee hichi Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

9
Sasa ambalo nataka, kwa wenye kujuwa hili
Wa Kenya na Tanganyika, na walo kulla mahali
Nipani ilo hakika, tubalegheshe ukweli
Nambiyani Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

10
Miye mefikiri mno, kuamuwa jambo hili
Na huona lugha hino, lazima ina asili
Kwa sababu kulla neno, lina mwanzo wa usuli
Ndipo ha'mba Kiswahili, hi lugha ya watu gani?

11
Na iwapo hivi sivyo, niliyyoamuwa hili
Nionyeshani viliyyo, mubainishe ukweli
Nijuwe ambavyo ndivyo, tutowane mushkili
Kifunuke Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

12
Na iwapo atakuja, wa kunijibu suali
Namuomba jambo moja, twambiyane kiakili
Tusionyane miuja, jambo nisilo kubali
N'anambiye Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

13
Tamati ndio akhiri, na jina langu ni hili
Ahmadi wa Nasiri, na Bhalo ndilo Ia pili
Mtungaji mashuhuri, mpenda penye ukweli
Nambiyani Kiswahili, ni lugha ya watu gani?

By Ahmad Nassir from Malenga wa Mvita
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom