I K SPORTS NEWS

I K SPORTS NEWS

Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga kinatarajia kuondoka leo jijini Dar es Salaam kwenda Mwanza tayari kuwavaa Mbao FC wikiendi hii.
Yanga wanasema wako kamili kwa ajili ya mechi hiyo lakini wamesisitiza hawatakuwa na dharau wala kuigopa Mbao FC.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Salum Nyika amesema wanaujua ubora wa Mbao kwa kuwa ni moja ya timu bora nchini.
“Kitu cha kwanza ujue ni timu ya ligi kuu, tunaiheshimu kama Mbao. Lakini si kwamba tunaigopa kwa kuwa tumejianda ana tuko tayari kwa mechi hiyo,” alisema.

Yanga imekuwa ikijifua bila ya Kocha wake, George Lwandamina ambaye alipata msiba wa kufiwa na mwanaye kwao Zambia.
images (4).jpg
 
YANGA KUIVAA MBAO FC BILA CHIRWA, UONGOZI WAMTETEA KUCHELEWA KUREJEA BAADA YA MGOMO




Uongozi wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, umesema mshambuliaji wake, Obrey Chirwa atareja nchini siku yoyote baada ya kwisha kwa msiba wa mtoto wa Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina.
Chirwa aliondoka nchini baada ya kuomba ruhusa kurejea kwao Zambia kwa masuala ya kifamilia. Lakini baadaye akagoma kurejea nchini akitaka kumaliziwa fedha zake za usajili.
Hali hiyo ilisababisha hali ya sintofahamu na Chirwa akaendelea kubaki Zambia huku akionekana mitandaoni akiendelea na kilimo cha mahindi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Salum Nyika amesema kilichomkwamisha Chirwa ni msiba wa mtoto wa kocha.
"Alikuwa bado Zambia, baada ya kusikia kocha ana msimba, alilazimika kubaki kule kumliwaza," alisema akionekana kutaka kupoza kidogo joto la Chirwa kubaki Zambia kwa mgomo.
Hata hivyo kumekuwa na taarifa kwamba, uongozi wa Yanga umemalizana naye kwa kumpatia kiasi cha fedha zake za usajili na umekubaliana naye kurejea haraka.
 

Miezi 15 iliyopita kiungobwa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast Yaya Toure aliutangazia ulimwengu kwamba anaachana na timu ya taifa ya Ivory Coast na kuelekeza nguvu klabuni.

Lakini sasa kiungo huyo ametengua kauli yake na kuamua kurejea tena katika timu ta taifa ya Ivory Coast katika kipindi hiki ambacho hana uhakika wa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Pep Gurdiola.

Wakala wa Yaya Toure bwana Dimitri Seluk amesema kiungo huyo amerejea katika timu ya taifa ya Ivory Coast sababu bado anaona anahitaji kushinda kombe lingine akiwa na timu ya taifa na sasa amerudi kulitafuta.

Yaya mwenyewe akielezea sababu kwanini amerudi katika timu ya taifa alisema “nalipenda sana taifa langu na nduo sababu nimerudi kama nitahitajika, ningependa kukisaidia kizazi kijacho kwa uzoefu nilionao”.

Yaya Toure alikuwepo katika kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast kilichoshinda michuano ya mataifa ya Africa mwaka 2015 na alifanikiwa kuichezea Ivory Coast mechi zaidi ya 100 huku mchezo wake wa mwisho ulikuwa September 2016.

Wakati huo huo wakala wa mchezaji huyo amesema Yaya hana mpango wa kuondoka Man City mwezi January kama inavyotajwa kwani ana mpango wa kushinda kombe lingine la EPL na klabu hiyo.
 

Simba, Yanga, Azam na Singida United zimeipangua ratiba ya Mapinduzi Cup inayotarajia kuanza December 29, 2017 kutokana na ratiba ya ligi kuu Tanzania bara ambayo itakuwa ikiendelea wakati mechi za kwanza za hatua ya makundi ya kombe hilo zitakapokuwa zikianza huku visiwani Zanzibar.

Ijumaa ya December 29, Azam watakuwa na mechi dhidi ya Stand United kwenye uwanja wa Azam Complex, Jumamosi kutakuwa na mechi tatu za VPL (Lipuli vs Tanzania Prisons, Mtibwa Sugar vs Majimaji, Ndanda vs Simba) wakati Jumapili Yanga watakuwa ugenini kucheza dhidi ya Mbao huku Singida United wao pia wakitarajia kucheza dhidi ya Njombe Mji.

“Ratiba kidogo iliingia utata kwa sababu Simba, Yanga, Azam na Singida United walipangiwa ratiba ya kucheza wakati kombe la Mapinduzi litakapokuwa limeanza lakini mechi zao tumezisogeza mbele.”

“Yanga wanaweza kuja tarehe 31 mwezi huu au tarehe 1 mwezi ujao, Azam watakuja mapema kwa sababu ratiba yao haiwakabi sana, Singida United na Simba nao watawahi kufika kati ya tarehe 1 au 2 mwezi ujao watakuwa tayari kuanza haya mashindano.”

“Kwa hiyo tuwaombe radhi wapenzi wa mpira Zanzibar kwamba, mechi za kombe la Mapinduzi zitaanza December 29, kwa kushirikisha timu za Zanzibar pekeake (Jamhuri, Mwenge, JKU, Zimamoto, Mlandege na Taifa Jang’ombe) halafu baadaye wataungana na timu za kutoka Tanzania bara. URA wanafika Dar December 29 kawawatafika mapema siku hiyohiyo wataunganisha Zanzibar au watafika kesho yake.”
 
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger leo atatimiza mechi 810 tangu aanze kuifundisha Arsenal - atakuwa anaifikia rekodi ya Sir Alex Ferguson.
26056005_1950923155221266_4429471139127381227_n.jpg
 
Pale unapogundua mzunguko wa kwanza umekwisha na mpinzani wako amekuacha kwa Pointi 15
1f600.png
1f600.png
1f602.png
1f602.png
1f602.png


 
MARQUIS NA TRAHSONI BURRELL WAOMBWA RADHI NA SHIRIKA LA NDEGE LA AMERICA, BAADA YA KUWASHUKU KUIBA BLANKETI

Shirika la American Airlines limewaomba msamaha wachezaji wawili wa mpira wa kikapu ambao walifukuzwa kutoka kwa ndege kwa kuwashuku kuiba.

Marquis Teague na Trahson Burrell walipanda ndege hiyo siku moja kabla ya krismasi wakielekea kucheza mechi.

Lakini kabla ya ndeye kuondoka uwanjani, muhudumu mmoja wa ndege alidai kuwa wanaume hao walikuwa mablanketi kutoka upande wa kifahari wa ndege ambapo walilazimishwa kushuka kutoka kwe ndege hiyo.

Baadaye ilibainika kuwa ni abiria walikuwa wamewapa mablanketi hayo.
Wachezaji hao wote walikuwa wa asilia ya Afrika akiwemo mhudumu wa ndege.
Hakuna mchezaji kati ya hao wanaochezea timu ya Memphis Hustle amezungumzia kisa hicho.

Laiki naibu kocha wa Hustle, Darnell Lazere aliandika katika twitter kuwa kitendo hicho kilichochewa na ubaguzi wa rangi.
Wachezaji walikuwa wakisafiri kutoka uwanja wa Dallas-Fort Worth kwenda Sioux Falls, South Dakota wakitumia ndege ya Envoy Air iliyo sehemu ya American Airlines.

 
BAADA YA ZAHIRI KUSAJIRIWA NA RUVU SHOOTING, NDANDA FC YAMTANGAZA NAHODHA MPAYA.

Benchi la ufundi la Ndanda SC limefanya Mabadiliko ya Nahodha wa Klabu ambapo awali Nahodha Mkuu alikuwa Rajabu Zahiri aliyehamia Ruvu shooting Na alikuwa akisaidiwa Na William Lucian Na Jeremia Kisubi.

Kwa Sasa Nahodha Mkuu atakuwa Jacob Masawe akisaidiwa Na

Salum Telela
Jeremia Kisubi
Hemed Khoja.

Haya ni Mabadiliko ya kawaida kufanywa Na Benchi la Ufundi Kwa Majibu wa Kocha Mkuu Malale Hamsini.

 
CARLOS CARVALHAL KOCHA MPYA SWANSEA CITY.

Klabu ya Swansea City imemtangaza rasmi kocha wa zamani wa klabu ya Sheffield Wednesday Carlos Carvalhal kuwa kocha wao mkuu.

Hii ni baada ya siku chache zilizopita kutangaza kuachana na aliyekuwa kocha wao Paul Clement kutokana na matokeo mabaya.

Kocha huyo Mreno anajiunga na Swansea mpaka mwisho wa msimu na kukiwa na kipengele cha kuongeza zaidi muda wa kuwa kocha wa klabu hiyo.

Kocha huyo wa zamani wa vilabu vya Besiktas, Sporting na Maritimo alichukua nafasi ya Stuart Gray katika klabu ya Sheffield Juni 2015 , ana wastani wa ushindi wa asilimia 42.7 katika mechi 131

 
Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi Tanzania Bara Boniface Wambura Mgoyo amesema kuwa kuna baadhi ya wachezaji waliosajiliwa katika dirisha dogo walikatiwa rufani na timu zao na sasa kamati ya Haki na hadhi za wachezaji imeketi kwa ajili ya kupitia rufaa hizo.

Wambura amewaambia waandishi wa habari kuwa wakati mzunguko wa 12 wa Ligi kuu ukiendelea kesho wachezaji hao huenda wakacheza ama laa na hiyo inatokana na kamati hiyo itakapoamua.

Aidha amesema kuwa zoezi la usajili lilifanikiwa kwa kiwango kizuri kwa mujibu wa Shirikisho la soka Tanzania hivyo wanaamini kila mchezaji na klabu zao watawatendea haki wachezaji wao.

 
Shirikisho la Soka Uganda (FUFA) limemtangaza #Sebastien_Desabre raia wa Ufaransa kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Uganda ( The Cranes).‬

‪Jumla ya makocha 92 waliomba nafasi hiyo ya kazi wakiwemo makocha 5 wazawa wa Uganda.‬

 
Back
Top Bottom