I love my wife but...

mimi huwa naamini sifa kuu ya mwanaume ni kuwa na busara na hekima/wisdom.napenda mwanaume anaeishi kiume.
sidhani kama mwanaume ambae ana busara anaweza kuwa tu anachatichati na maledies ovyo khaaa????

Halafu chating za usiku au baada ya kazi au darasani wakati una mke anakuangalia tuu ulivyo busy na simu
Yeye hata nafasi ya kuongea na wewe hana
Mmeshindfa mchana kutwa bila kuonana na ule muda anaopaswa awe na wewe uko busy na kisimu unachat na kuongea
Mimi nikifika home huwa sihanagaiki na kuzima simu naiweka mahali ambapo sitaikumbuka na hata marafiki na wafanyakazi wanajua muda wa kutuma ujumbe wao au kuchat na mimi
Nikishafika home simu na mimi ni mbalimbali ni muda wa kuwa na wife na watoto
Biashara ya kuambiwa aise lile file liko wapi baada ya muda wa kazi huwa halipo
 
Ukutane na mvivu kama mimi
Ukituma sms sitaijibu ila huwa naona kumaliza jambo nakupigia tuongee
Zile sms mia mbili siku nyingine nazipata saa tatu
Sasa mimi nitazitumia wapi
 
kuna watu wanaona simu ndo maisha mimi nikikupa no yangu utanichukia milele.sifagilii simu sana nipo selective sana kwenye watu wakuongea nao especially mida ya kupumzika.
 

Kwa hao wako walivyokuzoea sidhani kama kila siku wanakuita Maundumula
Lazima kuna kukuchombeza fulani wanakokupa
So we subiri kama BB yako unayoipenda hutaikuta kwenye sink la choo
 
Ukutane na mvivu kama mimi
Ukituma sms sitaijibu ila huwa naona kumaliza jambo nakupigia tuongee
Zile sms mia mbili siku nyingine nazipata saa tatu
Sasa mimi nitazitumia wapi
ahahaa mkuu saa tatu za usiku au?
 
kuna watu wanaona simu ndo maisha mimi nikikupa no yangu utanichukia milele.sifagilii simu sana nipo selective sana kwenye watu wakuongea nao especially mida ya kupumzika.

Unajua kuna watu sijui vidole vinawasha kutuma sms
Au kuchat
Unakuta amekutumia sms kukuuliza jambo na umemjibu
bado ataendelea kutuma sms ili akuvute uchat
Watu kama hao unawapotezea mbaya
Na Mkuu waaambie watu wako kuwa some time unahitaji muda na mkeo na kama una watoto pia upate muda na watoto wako
Kujua ni kipi kimetokea katika maisha yao kw asiku hiyo
Au mkeo akuambie ni yapi yalitokea wakati wewe haupo
 
ahahaa mkuu saa tatu za usiku au?

Saa tatu ndo may be nimetuma zile sms zao kumi na wananiambia eti umepata sms 200 za kutumia mpaka saa tano za usiku
Sasa mimi sms mia mbili nitazitumia wapi muda huo
 
Rocky,

Hizi ni changamoto za kimaendeleo zinaitwa, huu ulimwengu wa BB,fb,Hi5,Msn nk umefanya mawasiliano yamekuwa rahisi sasa kwetu wengine inakuwa changamoto.

Lakini mtu kuandika msg akasema"mambo vp dear" sioni kama ina tatizo unless atumie neno ambalo huwa mnaitana na mpenzi wako hahahaha hapo patachimbika
 
Saa tatu ndo may be nimetuma zile sms zao kumi na wananiambia eti umepata sms 200 za kutumia mpaka saa tano za usiku
Sasa mimi sms mia mbili nitazitumia wapi muda huo
ahahaaa hii mitandao kiboko. hizo offer wawape vijana watongozee
 



R' I see you see what I see.....
 

Sikatai huu ulimwengu wa mawasiliano kurahisishwa sana
Ila inategemea baada ya ujumbe kama huo ni habari gani zinafuata kwenye hiyo chating
Maana inaweza kuanza "mambo vipi dear" ikafuata statement nyingine ambayo kwa wife unaenda kujificha bafuni ili uisome
Sikatai kuna maneno kama hayo ambayo huwa ni utani na kuzoeana sana na mtu ila chunga sana hayo mazoea maana at the end kwa wife itakuwa story nyingine
 
mimi huwa naamini sifa kuu ya mwanaume ni kuwa na busara na hekima/wisdom.napenda mwanaume anaeishi kiume.
sidhani kama mwanaume ambae ana busara anaweza kuwa tu anachatichati na maledies ovyo khaaa????



IMO Kid sis hata wanaume busara fall in Love and Love chatting.... Sema kua mwanaume alo committed katika relationship iwe a serious galfriend ama mke na ana busara hutegemei ata chat ovyo ovyo na mabinti.
 
R' I see you see what I see.....

Yeah
Ila sitakubali na haitotokea
mambo ya ofsn yanabaki huko huko na hayana nafasi ninapofikia kuwa na wife na watoto
Huwa nakuna baba na mume kweli
Na hilo huwa nasisitiza sana na hata wao wanajua
 
Yeah
Ila sitakubali na haitotokea
mambo ya ofsn yanabaki huko huko na hayana nafasi ninapofikia kuwa na wife na watoto
Huwa nakuna baba na mume kweli
Na hilo huwa nasisitiza sana na hata wao wanajua
ndo maana nakulike mkuu
napenda sana mwanaume ambae yupo natural
i wish wa kwangu awe ivo?
 



Maundumula a person who is your dear ina maana mpo close.... Na hata kama ni mwanamke kakutumia message ya mambo dear mida mibovu uko na mkeo wakati hakutakii mema sababu nakuambia sie wanawake twajijiua na twaelewana. Huyo alotuma message kwako na kukuambia "mambo dear" akikuta the same message kwa mpenzi wake imetoka kwa mwanamke mwingine believe me you HATOPENDA; Anaweza asiongee lakini at the end of the day Hatopenda!

KWA NINI??

Mwanamke yeyote yule ambae sio mpenzi wako mkizoeana saana it is OK.... But in the long run mawazo ya Mapenzi ni lazima yatakuja kati ya hao wawili.... hasa kama wamezoeana, they understand each other, they blend na enjoy each other's company. Kuepusha hilo it is better kutojenga hayo kama tayari upo committed.... unless otherwise in the Long run mtake ku cheat will be inevitable for it is nature. Hivo in other words kama kweli hua wachat nao saa zote... it is bound to be flirting.... na one of the rule ya Flirtin if you are not serious..... Usiflirt na mtu mwaonana mara kwa mara ama mwashinda woote.... DANGEROUS!
 



Pole sana kaka!hapo kuna mambo mawili ambayo kwa upande wangu nayaona,
1).Inawezekana unakatabia ka kuiba nje ya ndoa na mkeo ameshtukia ila hataki kuwa muwazi kwako o lilishakuwaga varangati na hilo likaharibu imani ya mkeo kwako,au anaambiwa maneno mengiX2 na watu kuhusu wewe kwahiyo anakuwa hakuamini.na anamulika mwizi... kwa hiyo muweke chini mkeo zungumza nae kadiri uwezavyo ktk mazingira tofautix2,muulize kwanini hakuamini,kunatatizo gani?au anasikia nini?kutoka hapo utajua shida ilipo na wewe jitahidi ubadilike na mjengee imani kwamba umebadilika na fanya hivyyo kwa matendo.
2).Inawezekana mkeo wivu ndio tabia yake,au jinsi wewe unavyojiweka karibu sana na hao gelz kunamjengea picha tofauti,inawezekana kabisa wewe ukawa na kipaji cha kuzungumza,kufurahisha na kujua jinc ya kuwahandle gels,hilo likawa linawafanya wao wajisahau km wewe ni mume wa mtu na mara zote wakawa wanahitaji uwepo wako karibu yao,km ni hivyo ndivyo cha kufanya punguza sn kuwaweka karibu,na pili wakumbushe wewe ni mume wa mtu kwa hiyo wawe makini sana na hilo na zaidi ya yote waambie kwa uwazi kuwa mkeo hapendezwi na ukaribu wenu wa kihivyooooo kwahiyo mbaki kuwa marafiki mnaotafutana linapotokea jambo la msingi tn la msingi hasa,n kwa kufanya hivyo jua kabisa wengi watapungua maana tabia yetu wadada mtu akikufurahisha kidogo unajisahau km ni m2 wa m2 na pia jiandae kwa kuchukiwa maan ktk hali ya kawaida hao wadada watakuwa na interest zaid na hiyo nature yako.
Usijali wale watakao kaa mbali na wewe kwa kuwa muwazi kwao watakuwa hawakuwa na nia njema na wewe na mkeo.jikaze na uachane nao wanajamii forum tupo kwa ajili ya kusupportiana.......cheersss...
 
IMO Kid sis hata wanaume busara fall in Love and Love chatting.... Sema kua mwanaume alo committed katika relationship iwe a serious galfriend ama mke na ana busara hutegemei ata chat ovyo ovyo na mabinti.
by the way wanachati nini? wakipigwa mizinga wanaanza kulia. dawa yao ni kuwapiga mizinga tu naona,dear nitumie laki mbili kwa mpesa jamani tommorow is my birthday love youuuu.atacheua kweli hapo?
 
kweli sis hata maandiko yanasema ndoa na iheshimiwe na watu wote
kila mtu ni wajibu wake kuheshimu ndoa zilizopo duniani iwe ni ya kwako ,ya jirani yako,ya ndugu ,rafiki ,jamaa au ndoa tu yeyote .ni vema tukaachana na vuitabia vyote ambavyo ni hatarishi kwa usalama wa ndoa ,nadhani mojawapo ni hizo chitchat zisizokuwa na maana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…