I might be wrong, but I know I'm right

I might be wrong, but I know I'm right

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
NIlikuwa naangalia TVT hapa mara baada ya hotuba ya Rais Kikwete kwa Taifa. Mara kwaya ikatokea wakiwa wametilia sare zao za njano na nyeusi huku wakiimba wimbo uliokuwa ukisindikizwa na kinanda. Mwanzoni nilifikiri ni wimbo wa dini, lakini niliposikiliza nikaona wanaaimba nyimbo ya kumsifia mtu.

Kwa vile kwaya iliingia mara baada ya Rais miye nikaamini basi wanamuombea Rais kwa ajili ya mwaka mpya.. wanakwaya wakawa wanaimba kuomba baraka za Mungu juu ya mtu huyo kwa uongozi wake mzuri na kumtaka "Mungu amlinde" kwa mwaka ujao katika majukumu yake.. Niliposikiliza vizuri nikasikia jina la aliyekuwa anaimbwa na kuombewa Baraka... Tido Mhando wa TVT!

Now, I might be wrong, but I know I'm right.. ni matumizi mabaya ya chombo cha umma!
 
hehe Thats true

hata mimi nimeona.. alafu baadaye tido akawa anaongea hehehe
 
He!He! He!Mzee Mkjj hata wale vijana wa "Akudo" walimsifu na kumsalimia huyo kaka yako Mhando na TVT yake,nafikiri aloyafanya huko TVT si madogo!!!
 
Duuh, itabidi wamtungie hata ka-movie basi... ama kweli watu wanamapenzi...

Mkjj mimi pia nakutungia wimbo, nitaurusha TvT.... bora hata wangetumia muda wao kuangalia vikaragosi kwenye luninga (no offence)!!
 
Lakini?????
Ni sahihi kutumia TV inayo endeshwa kwa hela zetu kujitukuza???
 
NIlikuwa naangalia TVT hapa mara baada ya hotuba ya Rais Kikwete kwa Taifa. Mara kwaya ikatokea wakiwa wametilia sare zao za njano na nyeusi huku wakiimba wimbo uliokuwa ukisindikizwa na kinanda. Mwanzoni nilifikiri ni wimbo wa dini, lakini niliposikiliza nikaona wanaaimba nyimbo ya kumsifia mtu. Kwa vile kwaya iliingia mara baada ya Rais miye nikaamini basi wanamuombea Rais kwa ajili ya mwaka mpya.. wanakwaya wakawa wanaimba kuomba baraka za Mungu juu ya mtu huyo kwa uongozi wake mzuri na kumtaka "Mungu amlinde" kwa mwaka ujao katika majukumu yake.. Niliposikiliza vizuri nikasikia jina la aliyekuwa anaimbwa na kuombewa Baraka... Tido Mhando wa TVT!

Now, I might be wrong, but I know I'm right.. ni matumizi mabaya ya chombo cha umma!
Mzee mwanakijiji enzi hizo...
 
Uzi ulidorora sana huu!Vp tupe tathimini yako juu utukuzwaji unaofanyika sasa na chombo chetu cha TBC!
 
Kwa kweli sifa ziende kwa mwenyekiti wa maisha pale Ufipa.
 
Tukisema tuanzishe nyuzi za namna hii awamu hii si tutajaza server?
 
Back
Top Bottom