I miss Ander Herrera

I miss Ander Herrera

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,019
Reaction score
1,824
Nimemkumbuka huyu mtu --Ander Herrera -- alikuwa mmoja wa wachezaji ambao walipumua na kunywa maji ya bendera ya United haswaa!! na walionyesha mapenzi sana kwa timu kila anapoingia uwanjani alipambania timu hadi tone lake lamwisho la damu.

Sitasahau kamwe ile Derby ya Manchester alio piga goli kati kati ya uwanja pale Etihad Derby iliishia mguuni mwake, ama lipo mtengeneza Gerrard hadi kutolewa nje baada ya sekunde 38 tu hyu ndio Herrera bwana!

Unakumbuka alivyo muweka mfukoni na kumpoteza kabisa Eden Hazard Chelsea anakufa huku Herrera ana kila man of the match kwa goli moja assist na kumuweka Hazard mfukoni.

Sio tu kwamba Ander alikuwa imara kwa kukaba tu alifanya kazi zote chafu na safu yani tunaita full package midfield. Herrera yuko vizuri hata kwenye kushambulia,mtengenza nafasi na ni mfungaji mzuri sana.

Msimu wa 2016/2017 alimaliza akiwa ndio mchezaji mwenye assist nyingi zaidi pale matofali ya kuchoma, msimu ambao alichukua tuzo ya MUFC POTY(mchezaji bora wa msimu wa Manchester united).

Kilichotokea ni Edwoodward na jopo lake ndio wanakijua, kuanzisha mzozo na kuanzisha mgomo wa kumpa kandarasi kwa sababu walizo zijua wao.

Kilicho fata ni Herrera kutimkia PSG tena buree kabisa.

Herrera bado ana uwezo wa kiwango cha juu kabisa ni kwa bahati nzuri manchester kuna wachezaji wawili wazuri kati kati pale Fred na Mctominay ambao wameendeleza kila alichokianzisha Herrera.
 
Eti alimuweka Hazard mfukoni??

ushabiki na mahaba vinakupofusha

mechi ngapi mmepigwa akiwepo uwanjani??
 
Hana maajabu yoyote, ni mchezaji mzuri kama wachezaji wengine wazuri tunaowaona kila msimu. Viungo tunaopaswa kuwasimulia ni kama kina P.Scholes, Iniesta, Xavi n' the likes
 
Back
Top Bottom