I need to know the history of late leader of Kenya Mr George Saitoti

I need to know the history of late leader of Kenya Mr George Saitoti

Alikufa kwa ajali ya ndege ni kifo cha kawaida.
Hakikuwa kifo cha kawaida. 'Postmortem' ya mwili wa mwendazake pamoja na wengine wote ambao waliaga dunia, kwenye ajali hiyo, zilipatikana na chembechembe fulani kwenye mapafu. Ambayo iliashiria kwamba walikuwa 'exposed' kwa gesi flani hatari kwa afya wakiwa huko huko angani kwenye ndege. Jambo ambalo ndio labda lilisababisha ajali hiyo.

Kumbuka kwamba ajali hiyo ilisababisha pia kifo cha naibu waziri wake, Orwa Ojode kwenye wizara ya usalama. Baadae siku hiyo, kabla ya ajali, walikuwa wawasilishe bungeni majina ya watu mashuhuri nchini Kenya. Ambao walikuwa wanajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, yaani ma'don'.
 
Alikuwa mbunge wangu kule kwetu home Kajiado, toka nilipo zaliwa hadi alipoaga dunia. Yeye ndio makamu wa rais ambaye alikalia kiti hicho kwa muda mrefu zaidi ya wote. Mpenda amani. Profesa wa hesabu.

Wakenya tutamkumbuka kwa ile kauli yake ya hekima tupu; There comes a time.....when the country is more important than an individual! Baada ya rais mstaafu Daniel Arap Moi kumtema kama mrithi wake, kwenye mida ya lala salama ya utawala wake. Kisha Moi akamchagua kijana ambaye hakuwa anatambulika kisiasa wakati huo, yaani Uhuru Kenyatta. Hapo ni mukhtasari kwa ufupi. R.I.P Profesa.
Kifo chake kinadalili za mchongo?
 
Back
Top Bottom