I quit employment after reading this story and have never looked backed since,

hasa pale unapoamka saa 10 kuwahi foleni uwahi kazini na unatoka usiku unakutana na foleni hata watoto wanasahau kama wana baba au mama, ndoa nazo hazipewi kipaumbele kinachotakiwa, ili mradi umfurahishe muajiri mwisho wa siku namshahara hautoshi, ukipatra tu unalipa madeni, inakeraaaaaaaa
Isikuume take action!
 

Ni kweli Mkuu, Lazima uamke asubuhi upende usipende, na nilazima Urudi jioni sana upende usipende, Kazi mara zote ni Utumwa sema tu sisi huwa tunaona fahari sana Majirani, Ndugu, Jamaaa na marafiki kutuona tukifanya kazi, bila kujalisha hiyo kazi ina masirahi au la,

Wazazi huwa wanafurahi sana kusikia watato wao wamepata kazi na wanafanya kazi ofisini, na ndo maana nasema moja ya watu wanao rudisha nyuma kuenea kwa entreprenership Spirit ni wazazi, wazazi wana paly part kubwa sana
 
hi,
hii kitu imeniasha sana, inafurahisha
In short kazi haina maana sana ila wengi hatujui
 
hi,
hii kitu imeniasha sana, inafurahisha
In short kazi haina maana sana ila wengi hatujui

mkuu true kabisa, ukweli ndo huo, but kutoka huko ndo shughuli ni sawa na Mlevi wa Sigara kuja kuacha ni kazi kubwa sana
 
usianze kama jamaa wa kenya. ww anza biashara halafu ukizoea acha
 
usianze kama jamaa wa kenya. ww anza biashara halafu ukizoea acha

mkuu, utazoaje wakati husimamii biashara yenyewe? mi nadhani ili uzoee unatakiwa uwepo asubuhi hadi jioni ndio utaona mafanikio na vikwazo vyote. ukikaa ofisini na kuendesha biashara kwa remote utaendelea kuogopa kwamba kule hakulipi kutokana na mtu uliyemuweka huko, kumbe ungekuwepo mwenyewe ungejua namna gani ugangamale nayo.
 
Ujasiliamali unalipa kama ukijipanga vizuri na kama una bahati yako pia!!

Sure, na sacrifice pia. Ujasiriamali ni kujitoa muhanga, kwa maana ya kwamba unawekeza ili baadaye upate, regardless of the risks ahead.
 
Nasema bora uanze kuzoea mapema, ujasiliamali sio lele mama, kuna challenges nyingi sana, ukiacha kazi kabla hujaujua mapema utashindwa, biashara huwa inachukua muda kabla ya kuleta profit inayoeleweka, na kwa kipindi hiki mshahara ndio unakusaidia. anza kipindi upo likizo, ona challenges rekebisha mpaka uwe sawa yaani kieleweke
 
ndio unaingia full, the other alternative gather all information, jifunze unachotaka kukifanya, na ukijue ndani nje ongea na watu waliopo kwenye hiyo field kabla yako ikiwezekana angalia kabisa wanavyofanya chukua challenges chache utakazo ziona na uzifanyie kazi aas if kwamba upo kwenye hiyo biashara wakati huo hapo ndio ukiacha kazi na kuingia kwenye biashara moja kwa moja utaweza

Mwiko ni kumuweka ndugu, au mtoto, ukifanya hivyo jua boashara haina maisha na undugu utakuwa mashakani
 





Motivator:

 
usianze kama jamaa wa kenya. ww anza biashara halafu ukizoea acha

Ni kweli unatakiwa kuanza kidogo kidogo some time, Ila uzoefu unaonyesha kwamba wengi hufanya hivyo mapaka wanastafu, Mbona wafanya kazi kibao wana biashara zao?

Mimi nazungumzia full Entrepreners, ambapo hapa ndo kuna hitajika kufanya maamuzi magumu, Ila kama ni biashara za kuchuuza na kazalika hizo unapiga tu hadi ustafu ndo uwe full time.
 
Na kikubwa Ni Je unaridhika na Kazi unazo fanya? kama huridhiki nazo basi unatakiwa kutoka, make tumukuwa tukifanya kazi tusizo rizika navyo miaka hadi 30 unakutamtu tangia aingie hapo kazini ni kunung,unika mapka anastafu, sasa hapo ndo makosa yalipo,

Na kwa kifupi mfano mimi sioni umuhimu wowote wa mimi kuendelea kufanya kazi kwa sababu siko happy na kazi na napoteza muda mwingi na nguvu nyingi sana ambazo ningetulia kwenye kazi zangu ingekuwa ni faida kwangu, Sometime si kwamba watu wanaacha kazi kwa sababu wameisha kusanya pesa ya kutosha, no ni kwa sababu wanaona hakuna wanacho faidi,

Unakuwa mtumwa wa kuhesabu siku, ili Mwisho wa mwezi upate pesa, Unakuwa kila siku ni mtu wa kumuuliza mhasibu wenu kama amesiha peleka mishahara Benki, haya ni mambo ambayo kwa binafisi sioni mantiki yake,

Jiulize ni Miaka mingapi sasa uko Kazini na kuna Cha maana umefanya katika maisha yako? Kwangu mimi naona hakuna, Tatizo watu tunakuwa na uoga kwamba sasa ndugu zangu watanielewa vipi? Mke/Mme wangu atanielewa vipi? Mcumba wangu atanielewa vipi? si ndo atanikimbia? Majirani Je? Marafiki Je? Nisha zoea kufuatwa na Gari la Kampuni sasa itakuwa vipi? Ofisini mimi ni Bosi sasa itakuwa vipi? Vile viyoyozi vya Ofisini kweli niviache?

Ukisha fikilia hayo yote ndo inakuja ishu ya kwamba ngoja nifanye kwanza, Mkuu Ajira ni sawa na mtu amabye amedata na sigara, au Pombe kuacha ni shughuli,

Wapo wengi walio apa kwamba wanaajiriwa miaka Miwili, au Mitatu au Miatano then wanatemeana na kazi na wanajiajiri But mpaka sasa wana miaka 20 wakiwa huko huko,

SO KUCHUKUA MAAMUZI KAMA YA MUGUKU NI WEWE MWENYEWE UKIONA HAIWEZAKANI UNACHAPA KAZI, KWA SABABU HATA HIVYO HAIWEZEKANI WOTE WAKAWA WAJASIRIMALI, HATA NCHI KAMA INDIA, CHINA, ambazo zina rate kubwa sana ya Entreprenership Spirit still kuna watu hawataki kusiki kitu Kuwa wajasirimali, so sio Tz pekee bali ni kila mahali
 
asante mkuu shache kwa somo zuri, hakika nimepata kitu hapa
 
kipindi hiki ukiacha kazi ili uwe interprenuer inakula kwako
UD

Wahanga wa kujiriwa, wewe ndo wale mkipunguzwa ghafla unapata ugonjwa wa Moyo, na ulicho sema ni sahihi ni lazima uwatumikie mabwana upate kula,

NARUDIA JAMAN UJASIRIMALI SI KWA KILA MTU, WENGINE TUENDELEE NA AJIRA ZETU KWA PAMOJA TUTAJENGA TAIFA LA TANZANIA

 
Wafanyakazi wengi wanapenda kuwekeza (Investing ) hela ya mshahara ili kwamba ata biashara ikikata basi anakuwa hadaiwi na mtu ambapo sio sawa na kuwekeza hela ya kukopa benki ambayo ikitokea biashara imekata utadaiwa kwa nguvu mpaka ulipe yote.Sasa ukiwekeza hela yako mwenyewe wala unakuwa sio mtumwa wa kutafuta faida kwa nguvu kama vile ingekuwa umekopa, na hapo ndipo utakuta biasharg ipo ilimradi ipo hata haikuwi kwa sababu hakuna kinachokushurutisha.
 
Haaaaaa nikipunguzwa kazi nitapewa kiinua mgongo na pia nikiongeza na ppf/nssf yangu nakuwa na pesa za kutosha hivi zisizopungua mil30 kama nitapunguzwa sasa so sijawahi ogopa kufukuzwa kazi, nitaanza bizness mda ukifikia lkn si kwa kuacha kazi
 
Mkuu hio ni theory, wewe mpaka uje ustafu ukiw n miaka 60 ndo unze Business ka faida ya nani? kwai hatuwaoni Kitaa? natmikia Taifa au Kmpuni mika 30 hadi 40 ukistafu unaishiakuapta Milioni 50, piga huo muda wot na miaka yote kama ungewkezaktka biashara yako ungekuwa wapi?

Ndo maana MUGUKU alisema kama angeendela na kzi ya Kuajiliw asingekua hapo alipo, na yeye aliamua KCHOMA MELI moto si kwamba hakujua kwamba mbeleni kuna nini, na kwa maelezo yake alikumbana na vikwazo vingi saa ikwemo kukatishwa tamaa,

Mkuu wake wa chuo/bosi alimkatisha tamaa, Wazazi wakewalimwabia atakuwa amechanganyikiwa kwa uamuzi w kucha kazi, hata mtaani ni hivyo hivyo, Kuna Rafiki yangu mmoja yeye alikuwa akisoma CBE Dodoma mara tu ya kumaliza Chuo aliingia kijijini kwao kuanza Ujasirimali, waliimwongea sana kuanzia ndugu, Jamaa, watu wa Kijijini kwao na walimuona kama karukwa na akili na wengine walisema atakua amefel ichuo, na wengine kushangaa Graduate kurudi Kijijini, Ila ninavyo andika wale walikuwa wakimshangaa kwa sasa wanarudi kuomba kazi kwake,

Kwa kifupi ndo hivyo ilivyo, THOMAS EDSON aliambiwa na mwalimu wake kwamba yeye katika maisha yake hawezi kufanya chochote kile na mwalimu wake alimuona kama mtu mjinga lakini unajua kilicho kujakutokea,

MICHAEL JORODAN, Mcheza kikapu alitemwa kwenye timu ya basket ball ya chuo kwa kumuona hawezi chochote na alishindwa majaribio zaidi ya 500 laikini mwisho w siku alikuja kuwa kama alivyo

 
Chasha usidanganye watu ebu weka jina lako halisi na ulikuwa unafanya kazi wapi na ulivyoacha umfanikiwa kwa kiasi kipi hicho? usije kuwaingiza king vijana wenzako.
 
Last edited by a moderator:
Nimefarijika sana na uzi huu ! Sijawahi ajiriwa kwa hiyo sijui ladha yake , Yes kuna challenge zake kwenye kujiajiri lakini kwa upeo wangu ni bora kuliko kukaa kwenye kazi isiyo na maslahi. Kimsingi unaweza kupanga mambo yako vizuri kama umejiajiri kwa sababu huwi chini ya mtu tena . holiday ni siku yoyote unayoona umechoka na kazi ni siku yoyote unayoona uko kwenye mood ! huwa najiuliza kwa nini waajiriwa wengi wanapostaafu hufikiria baishara , tena wakitumia mafao kama mtaji? Kwa walio ajiriwa kama unataka kuwa mjasiamali itabidi ufanye marekebisho ya marafiki hadi majirani ili usipate upinzani hasa wa kisailolojia, halafu ujiamini na kukubali kila challenge ,utafanikiwa tu. Nawashangaa wanaosema eti kujiajiri si lele mama! Nadhani kuajiriwa ndo sio lele mama , umfikirie bosi, pesa mwisho wa mwezi , udamke saa kumi kwa walio dsm kurudi saa 4 , kugombea vyeo n.k na bado ukistaafu ufikirie BIASHARA YA KUFANYA !!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…