I Sympathize with Habib Kiombo Simba mmemkosea sana Habib Kiombo

I Sympathize with Habib Kiombo Simba mmemkosea sana Habib Kiombo

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Mimi ni shabiki wa damu wa Dar Es Salaam Young Africans lakini hiki kilicho tokea kwa kijana mwenzetu Habib Kiombo kimenigusa sana.

Habib ame twezwa.

Anacho fanyiwa Habib ni public humiliation.

Anahukumiwa yeye kwa makosa ya viongozi na PR wa simba.

Kama kijana anae tafuta maisha yake kupitia mpira wa miguu sidhani kama atakuwa ana furahishwa na Maneno ya kejeli kutoka mashabiki wa Simba na Yanga wa mitandaoni.

Tuweke ushabiki pembeni, mwana atakuwa anapitia kipindi kigumu sana cha maisha yake.

Habib Kiombo sio mchezaji mbaya la hasha. Ni mchezaji mwenye uwezo mzuri tu uwanjani. Ukiona mchezaji anasajiliwa na Simba na Yanga basi uwe na uhakika kwamba ni mchezaji mzuri.

Tatizo ni poor choose of time ya kumtambulisha.

Habib sio mchezaji mbaya isipokuwa ametambulishwa katika kipindi kibaya.

Watu wa PR wa Simba wamemtambulisha Habib bila kuziheshimu siasa za Simba na Yanga.

Kwa siasa za Simba na Yanga, mashabiki wa Simba walitegemea leo angetambulishwa mchezaji wa kigeni mwenye jina kubwa au kama ni mchezaji wa hapa hapa bongo basi at least awe yule aliye fanya vizuri kwenye msimu ulio pita mfano George Mpole.

Unapo fanya matangazo makubwa kiasi hicho kuwatamanisha mashabiki wa klabu yako kwamba utakwenda kisimamisha Afrika halafu una mtambulisha mchezaji anae toka kwenye timu iliyo shuka daraja lazima utegemee kupata backlash kutoka kwa mashabiki wa Simba na Yanga.
Simba walitarajia kuletewa Rachel ( Genesis 29:18) lakini wakaishia kupewa Leah ( Genesis 29:25)

Mwisho wa siku kejeli zinaenda kwa kijana wa kitanzania anae pigana kutafuta ugali wake.

Simba wangeweza kutangaza majina makubwa mawili au moja halafu baada ya hapo ndo wakamtangaza Habib. Hivyo ndivyo siasa za Simba na Yanga zinavyo taka.
Hata hivyo Mungu ni wa ajabu sana. Huyo huyo Habib Kiombo ambae mashabiki wa Simba na Yanga wana mkejeli , anaweza kuwa mchezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika ardhi ya Tanzania. Siku zote Mungu huwa anapenda kusimama na watu wanao chukuliwa kuwa hawawezi ( 1 Samuel 16:1-13)

Even the internet was created without internet.

Hata Wenger aliwahi ' kupigwa mawe' kwa sababu ya usajili wa Nicolas Anelka na baadae Thierry Henry.

Wenger huyo huyo aliwahi kumkataa Ronaldo, kilicho tokea kwenye career ya Ronaldo baadae hata Zuchu ana kijua.

i Sympathize with Habib Kiombo.

Habib Kiombo take heart. The Lord God is with you.

U shall be successful in ur career.
 
Nyie endeleeni kuchezea shilingi chooni, Kwa usajili mnao ufanya zipo Dalili za timu kushuka Daraja.
Sasa msitegemee Yanga awe anafanya kazi ya kuwabeba Ili msishuke Daraja kama Walivyo fanya 1989. Acheni siasa fanyeni usajili, msimu ujao ni mgumu kuliko huu ulio Isha.
Mtakuja kumlaumu Karia bila Sababu.
 
Lengo lako ni ubishani au ukweli?
weka facts, Kosa la Ahmed ni kufanya promo (ambayo ni kazi yake)? BTW hata wewe nakutaka twende kwa fact na sio ubishani.
Mwisho wa siku mchezaji ataonyeshe vitu uwanjani na sio ukubwa au udogo wa promo
 
weka facts, Kosa la Ahmed ni kufanya promo (ambayo ni kazi yake)? BTW hata wewe nakutaka twende kwa fact na sio ubishani.
Mwisho wa siku mchezaji ataonyeshe vitu uwanjani na sio ukubwa au udogo wa promo
Kabisa umeshupaza shingo hulioni kosa la Ahmed?

Tention kama ile umewaweka mashabiki ni level na surprise ya kumrudusha kama Konde Boy, au umepinduwa meza kwa Aziz Ki na siyo kwa mtu aliyetoka Mbeya na Super Feo.

Ndio sababu watu wa Simba wamekuwa disappointed na hasa ukichukulia upande wa pili watu wana furaha na mambo yanakwenda super
 
Kabisa umeshupaza shingo hulioni kosa la Ahmed?

Tention kama ile umewaweka mashabiki ni level na surprise ya kumrudusha kama Konde Boy, au umepinduwa meza kwa Aziz Ki na siyo kwa mtu aliyetoka Mbeya na Super Feo.

Ndio sababu watu wa Simba wamekuwa disappointed na hasa ukichukulia upande wa pili watu wana furaha na mambo yanakwenda super
Wanajua Simba wengi ni mbumbumbu, wanafanya watakavyo tu 🤣🤣🤣
 
Tatizo mashabiki wengi ni wale jobless graduates, wana hasira kinyama utadhani simba na Yanga ndo waliowanyima ajjra.
Inafika mahali unajiuliza, haka ka jamaa kamewekeza sh ngapi pale simba kwamba katapata hasara??

"Yote 9, hii mainstream imejaa mabogus"
 
Back
Top Bottom