Elections 2010 I.t.v bado inalo deni kubwa kwa watanzania

Byendangwero

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2010
Posts
871
Reaction score
56
wana-jamii forum mpo? mimi ndipo hivi sasa najiunga kundini. Naomba nianzae kwa kutoa maoni yangu kuhusu mdahalo wa jana wa Dr. Slaa. Awali ya yote napenda niupongeze uongozi na watendaji wa I.T.V kwa kutoa uwanja ulio mwezesha mpenzi wetu na raisi wetu mtarajiwa kuwasiliana moja kwa moja na maelfu ya wapiga kura wake. Pamoja na pongezi hizo, napenda niseme tu kwamba I.T.V haikuonyesha kiwango cha weledi kilichotarajiwa katika kutekeleza jukumu hilo. Hii inatokana na ukweli kwamba habari yeyote ile huwa na sura mbili; sura ya kwanza ni ya mtoa habari mwenyewe, na sura ya pili ni ya hao wanao ipokea hiyo habari. Jana I.T.V imetuonyesha sura moja tu ya mtoa habari na haikujushugulisha hata kidogo kutuonyesha habari hiyo iliyokuwa inatolewa ilipokelewaje na umma wa Watanzania. Kwa maoni yangu, hii ni kasoro kubwa sana ambayo I.T.V inapashwa ifanye kila linalo wezekana kuisahihisha kwa gharama yoyote ile vinginevyo umaarufu wa chombo hicho utakuwa umeingia doa kubwa.
 
samahani kidogo sijaelewa......ulitaka ITV ionyeshe na watazamaji?...mh mi mbona kama naona ujumbe ulifikishwa ipasavyo....au una maana gani?....karibu jamvini anyway
 
Uko sawa ,hapa jamaa hawawezi kukuelewa maana wamezoea spoon feeding,kwanza nataka ujue kuwa Dr slaa alikuwa amepewa maswali na rose ndo maana wakati anajibu maswali alikuwa anasoma karatasi na kuonesha kuwa majibu alikuwa nayo nazani watanzania wanapaswa watoe feedback kwa mtazamo Dr slaa anaweza kuwa Rais Dictator na kuitumbukiza nchi hii katka mACHAFUKO KWA KUWA MALA ZOTE ANAONESHA KUWA MLIPIZA VISASI NA HILI NI TATIZO KWA KIONGOZI WA JUU,HAFAIIIIIIII KABISA KUWA RAIS NA HATA SHINDA.
 

badfo hamjakata tamaa tu, du mna roho ngumu ama ndio kulipa fadhira kwenyewe hukko?
 
Hawa jamaa wana roho ya paka hawataki kuukubali ukweli kuwa Dr. (Waukweli) Slaa ni unstoppable! Kuhusu ITV ni kweli walipaswa kuweka pia maoni ya watanzania ama kwa kuwa na wanataaluma kujadili mdahalo huo baada ya kumaliza au kuongea na watu wameupokea vipi ujumbe wa raisi mtarajiwa.
 

hivi wewe uko sawasawa kweli, mbona unataka kuongopa mchana kweupeeeeeeeeeeee
 
Mkuu hapa nadhani ulimaanisha kuwa pengine zingeruhusiwa simu walau mbili au tatu kutoka nje ya wale waliokuwa naye au?
 
Karatasi ile ni ya ku-note maswali ya waulizaji tuu. Majibu yalikua yanatoka kichwani kwake yakiwatia homa mafisadi kama wewe.
 
Nimekuelewa brotha hii kwa ukiritimba wa serikali yetu nina uhakika wanaweza fungiwa wakifanya hilo yaani imepokelewa vp?
 
Uko nje ya mada mkuu, Ni vizuri ukajadili mada iliyoanzishwa na wenzako pia na si kuchomekea mambo yako popote pale hata mahali ambapo hayaitajiki. Kama vipi anzisha thread yako tuijadili.
 
JK na Babu Seya
 
he, umeona ile ID yako haikufai sio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…