Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
wana-jamii forum mpo? mimi ndipo hivi sasa najiunga kundini. Naomba nianzae kwa kutoa maoni yangu kuhusu mdahalo wa jana wa Dr. Slaa. Awali ya yote napenda niupongeze uongozi na watendaji wa I.T.V kwa kutoa uwanja ulio mwezesha mpenzi wetu na raisi wetu mtarajiwa kuwasiliana moja kwa moja na maelfu ya wapiga kura wake. Pamoja na pongezi hizo, napenda niseme tu kwamba I.T.V haikuonyesha kiwango cha weledi kilichotarajiwa katika kutekeleza jukumu hilo. Hii inatokana na ukweli kwamba habari yeyote ile huwa na sura mbili; sura ya kwanza ni ya mtoa habari mwenyewe, na sura ya pili ni ya hao wanao ipokea hiyo habari. Jana I.T.V imetuonyesha sura moja tu ya mtoa habari na haikujushugulisha hata kidogo kutuonyesha habari hiyo iliyokuwa inatolewa ilipokelewaje na umma wa Watanzania. Kwa maoni yangu, hii ni kasoro kubwa sana ambayo I.T.V inapashwa ifanye kila linalo wezekana kuisahihisha kwa gharama yoyote ile vinginevyo umaarufu wa chombo hicho utakuwa umeingia doa kubwa.