Jamani sijakurupuka. Nimefikiria sana. Ni rahisi kusema kwa mdomo au kuamini moyoni, lakini ni ngumu kuigiza kutenda. Wapo wanaoimba kila asbh na jion nakupenda na tena wanaamini hivyo lakini wanatenda sivyo. Hivi hamjawaona watu ambao hawaguswi pale wanapowaudhi wenzao. Wapo ambao hawajisikii chochote wakiwaona wake zao wamekasirika, lkn wanaimba kila saa I love You. Wapo wanaojisikia raha zaidi wakila nyama choma baa kuliko kilichopikwa na wake zao lkn wanaamini wanawapenda wake zao. Wapo wanaopeleka nyama kwa nyumba ndogo na mke anakula maharage lkn wana uhakika wanawapenda wake zao. Wapo wasiopenda hata kuandamana na wake zao njiani japo wanasema wanawapenda. Nimejaribu kujifikiria vile najisikia vibaya mke wangu akiudhiwa, ninavyopenda kumuona ana raha, ninavyojitahidi kuepuka kumuudhi, na kubwa zaidi ninavyojisikia raha ninapomwona pembeni yangu. Najua hata hivyo inawezekana vile mi nafanya, sivyo ningetakiwa kufanya. Ndio maana n