Mama atiwa mimba na mwanaye
Mjane mmoja wa kijiji cha Mwenezi nchini Zimbabwe, aliyejulikana kwa jina la Betty Mbereko (40), aliyetiwa mimba na mtoto wake wa kumzaa, Farai Mbereko (23) na kuutangazia umma kuwa anataka kufunga naye ndoa amefukuzwa katika kijiji hicho...
Betty amefukuzwa na uongozi wa kijiji kutokana na maelezo kuwa kitendo cha kupewa mimba na mtoto wake wa kumzaa ni cha kinyama na ni kinyume cha maadili ya kabila lao.
Tukio la kutiwa mimba kwa mama huyo limetokea mwanzoni mwa mwezi huu na kuripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini Zimbabwe, ambapo uamuzi wa wawili hao kutaka kuoana ulipingwa vikali na ndugu, jamaa, pamoja na serikali ya kijiji.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mwenezi, Nathan Muputirwa aliipinga ndoa hiyo kwa kusema: Hatuwezi kuruhusu hili kutokea kwenye kijiji chetu, ni dalili mbaya, ingekuwa zamani, watu hawa wangeuawa, lakini leo hatuwezi kuwaua kwasababu tunaogopa polisi
Pamoja na upinzani huo, mtoto wa mjane huyo, aliendelea kudai kuwa, yuko tayari kulipa mabaki ya mahari ambayo marehemu baba yake alikuwa hajamalizia ili aweze kummiliki mama yake, huku akimsifia kuwa ana mvuto sana wa kimapenzi.
Nampenda sana mama yangu, kwani yuko very sexy, na nitamalizia ile mahari iliyobaki kabla ya kifo cha mzee, ili nimuoe, alisema Farai.
Hata hivyo, serikali ya kijiji iliwataka wawili hao kuchagua kati ya kusitisha ndoa hiyo au kuhama kijiji na wao wakachagua kuhama na kuelekea kusikojulikana.