kweli alichukuaga watoto ila huyo mdada alienda mahakama ikampa watoto baada ya kupeleka vielelezo vya kuthbtisha mwanaume anawatesa na kuwanyanyasa watoto.Na ilikuwaje mwanaume mkorofi hivyo amruhusu huyo dada aondoke na watoto? Mimi nijuavyo sheria ya Tz mama hana mamlaka na watoto kwa hiyo ninge expect huyo jamaa ang'ang'anie watoto kama njia ya kumrudisha wife. Imekuwaje kamruhusu aondoke na watoto? I am trying to think what kind of a man he is. Kwa experience yangu wanaume makatili kama yeye chakwanza anachofanya ni kukunyang'anya watoto; sasa hapa naona different story!
Avichinje vitoto na yeye anywe sumu story iishie hapo.Nina rafiki yangu alitengana na mumewe kwa miaka 6 sasa na mwaka jana wamepeana talaka rasmi.Huyu dada ni m2 strong sn kwani alipotelekezwa alijikaza akajisomesha huku anatunza watoto wake na sasa yuko chuo kikuu mwaka wa pili. Kuna ki2 kinamtesa dada huyu yani akipata mwanaume mtalaka wake huwa anaingilia mahusiano hayo ingawa alishaoa mke mwingne. Miaka 2 baada ya mwanaume kumwacha alipata mpenz jamaa alipockia akamvizia yule kaka akampiga sn so dada akamwagwa, mwaka mmoja bdae tena akapata mwingne nae akatishiwa akamwagwa tena, akaona bora apate talaka ndio atakuwa huru, mwaka jana walitalikiana ila mambo ndio yamekuwa mabaya zaidi, yule kaka alimwapia akiwa na m2 mwingne atamuua kwan ye bdo ni mkewe kwan walifunga ndoa kanisani na ndoa ya kanisani haifi. Akamwambia atamtesa hadi amrudie ila kwa vile dada ni strong akamwambia afanye atakavyo bs kaka yule ameanza kuchawia watoto aliokuwa amezaa na yule dada (watoto wanakaa na mama) anawapiga watoto wake majini, wanamsumbua sn huyo dada. Sasa amechoka hana raha tena kwani shule hasomi kwa raha kwani watoto wanaugua ugua (kipepo, wakipelekwa kwa walokole wakiombewa wanapona) akipata mwanaume wanatishiwa wanamuacha, amekuwa mpweke na anakaribia kuchanganyikiwa. Amepanga ki2 kibaya sn na amenishirikisha nikaogopa ndio mana nikaleta hapa jamvini kwani anataka kumrudia mtalaka wake kwa siri then cku moja amtaftie wahuni wamfanyizie. Nimeogopa na kuona madhara ya hlo jambo ila ndio alichoamua. Alisema maneno haya "NILIMPA MOYO WANGU, MAISHA NA WATOTO, SASA ANATUTESA, ANATAKA TUFE, BORA ANITESE MIMI KULIKO WATOTO WANGU, WAMEMKOSEA NINI? I'LL KILL HIM 4 MY KIDS" ushauri wenu plz NITAMSHAURI NINI AACHE WAZO LAKE? Nisaidieni plz
Pole zake huyo dada! Hilo analotaka kufanya si njema kabisa kwa maisha yake! Ni bora autafute msaada kwa Mungu, hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Akitulie kwa Mungu, Mungu atamsaidia kumdhibiti huyo mwanaume, na kamwe hatamfanya kitu chochote!
That is very true.mwanaume mkatili hivo hung'ang'ania watt.lkn jamn wanume wa jinsi hii wapo tena kwenye jamii yetu hii hii.i have met one.ukihadithia mtu anaona kama unaeleza yasiyowezzekana but ni kweli.unakuta wanaume wa jinsi hii ye anakuwa ni mtu wa kuoa na kuacha.kila mwanamke kwake anamatatizo.ila ye hana.wanaume wa jinsi hii jaman wapo msibishe!Na ilikuwaje mwanaume mkorofi hivyo amruhusu huyo dada aondoke na watoto? Mimi nijuavyo sheria ya Tz mama hana mamlaka na watoto kwa hiyo ninge expect huyo jamaa ang'ang'anie watoto kama njia ya kumrudisha wife. Imekuwaje kamruhusu aondoke na watoto? I am trying to think what kind of a man he is. Kwa experience yangu wanaume makatili kama yeye chakwanza anachofanya ni kukunyang'anya watoto; sasa hapa naona different story!
Nimependa sana hadithi yako dada.imenitia moyo sana.stori yako haina tofauti na yangu.lkn je ina maana watt hawamjui baba yao halisi?pole sana dada nahuzunika sana nikikumbuka hapo.nafsi yangu inalia!dunian tunapita.ipo siku tutasahau machungu haya!Miaka 12 iliyopita nikua kwenye hali ngumu na mbaya naweza kusema kuliko yake, na Mungu alinisaidia baada ya kuamua kumsamehe yule mwanaume na kutokuangalia yale mabaya aliyonitendea, tuliachana nae 1999, akaniachia watoto, mmoja mwaka 1 na miezi 8 mwingine miaka minne, sina pesa sina kazi sina pa kulala. Nilianza kwa kulala chiniNiliamua kumtumika Mungu na kufanya kazi kwa bidii niweze kuwalea watoto, Ilikua kila nikikumbuka alivyonioa kwa arusi nzuri na mateso anayonipa ninalia tu. Miezi sita baada ya kuachana nae niliamua kumsamehe na kumsahau, hata akifanya nini nakua kama simuoni, Nilimuomba Mungu aondoe kumbukumbu yoyote kuhusiana na huyu jamaa. Baada ya mwaka yule jamaa alipata matatizo ikabidi arudi kijijini, Mungu akawa ametuweka mbali hatuonani. Kuanzia wakati huo mpaka leo sijawahi kumuona.Na Mungu alinisaidia miaka mitatu baadae nilikua tayari na curio shop yangu na nimeweza kujanga kanyumba kakuishina watoto wanasoma shule nzuri,miaka Kumi baadae nimeolewa na mwanaume mwingine na anasomesha wale watoto wake.Story ni ndefu lakini kwa ufupi huu unaweza kupata picha.Ushauri wangu kwa huyu dada, Kwanza naona ni mpiganaji, kwa hakika najua atashinda:Kwanza huyo dada aombe rehema kwa Mungu na atubu kwa yote, maana kabla ya kuolewa na huyo jamaa inawezekana Mungu alikua anamuonya na hakusikia au hakujua. Aombe rehema kwa Mungu. Zaburi 71 iwe sala yake itamsaidiaPili, ajiunge na huduma yoyote kanisani amtumikie Mungu kwa moyo wake wote huku akiomba kwa bidii kwa ajili yake na watoto wake.Tatu Ajitahidi kumfuta huyo jamaa kwenye moyo wake na mawazo yake, amuombe Mungu asiwakutanishe hata njiani Zaburi 35 yote. Aweke maisha yake kwa Mungu na amuombe Mungu ampe Mume wa kweli na siyo mpenzi au rafiki wa MudaAishi Maisha safi ya utakatifu. Siku si nyingi Mungu atakutana nae.Mungu ni mwaminifu, atashangaa jinsi atafanya miujiza na kila kitu kitabadilika bila hata yeye kupambana sana.Mkabidhi Bwana njia zako umtumaini nae atafanya.Let her hold unto God he will never live her alone. Malaika wake watapigana kwa niaba yake. Vita ni vya Bwana.Dada haya ninayokwambia yanatokana na yale niliyoyapita kwenye maisha, na wala sikuwa msomi wala kupata bahati ya kwenda shule kama yeye. Lakini Mungu amenitoa utukufu hadi utukufu.Siwezi kusema yote hapa ila Najua Mungu atamsaidia, Asimfanyie huyo jamaa chochote amkabidhi kwa Mungu.
Sio wa kuambiwa akazane na masomo kwani anakazana kweli! Hlo nje ya nchi sidhani km litawezekana labda apate scholarshp ya nguvu.Mwambie huyo dada akazane na masomo yake aache kutafuta mtu wa kumwoa kwa sasa. Afaulu masomo yake halafu akimaliza atafute shule nje ya nchi aondoke na watoto wake na asirudi nchini mpaka asikie huyo bwana hayupo duniani. Huko sasa atafute wa kumliwaza. Ujinga unamsumbua huyo mwananume
Nimependa sana hadithi yako dada.imenitia moyo sana.stori yako haina tofauti na yangu.lkn je ina maana watt hawamjui baba yao halisi?pole sana dada nahuzunika sana nikikumbuka hapo.nafsi yangu inalia!dunian tunapita.ipo siku tutasahau machungu haya!
Kwa kweli ningesafiri hadi nigeria kama si kutafuta na mie nguvu hizo basi kwa mtume joshua, angenisaidia tu, huyu mwanaume katokea sayari gani wajameni, sijawahi ona, mke amwache mwenyewe, wivu wa nini?
Hapo ndio ninaposhangaa kwa tabia fulani za kibabe ambazo hazina msingi wowote,..mwanamke umeachana nae tena muda mrefu_umepata mwanamke mwingine na kuoa lakn unataka mwenzio asiolewe wala kuwa na mpnz,...huu ni upuuzi , unyanyasaji,ukatili,ubinafsi,ubabe,na ujeuri uliopindukia wa kuthamini furaha na heshima yako bila kujali furaha na heshima ya watu wengine.
Kuhusu hilo suala la kuroga watoto...hapo sitii neno kwani siamini sana kama mtu kweli anaweza kuloga watoto tena watoto wake wasio na hatia hata chembe,....ila inawezekana tu kwa mtu mkorofi na jeuri wa aina ya huyu jamaa.
Muda mwingine sisi wanaume pengine hatuwatendei sana haki hawa wapenzi wetu......tunawaumiza sana na inatia hasira na uchungu sana kama angekua dada ako sidhani kama akifanyiwa hivyo kama utaridhika,......makosa mengine pengine yanastahili adhabu ya kifo,....nimenuna na kukereheka sana na tabia hii