Miaka 12 iliyopita nikua kwenye hali ngumu na mbaya naweza kusema kuliko yake, na Mungu alinisaidia baada ya kuamua kumsamehe yule mwanaume na kutokuangalia yale mabaya aliyonitendea, tuliachana nae 1999, akaniachia watoto, mmoja mwaka 1 na miezi 8 mwingine miaka minne, sina pesa sina kazi sina pa kulala. Nilianza kwa kulala chiniNiliamua kumtumika Mungu na kufanya kazi kwa bidii niweze kuwalea watoto, Ilikua kila nikikumbuka alivyonioa kwa arusi nzuri na mateso anayonipa ninalia tu. Miezi sita baada ya kuachana nae niliamua kumsamehe na kumsahau, hata akifanya nini nakua kama simuoni, Nilimuomba Mungu aondoe kumbukumbu yoyote kuhusiana na huyu jamaa. Baada ya mwaka yule jamaa alipata matatizo ikabidi arudi kijijini, Mungu akawa ametuweka mbali hatuonani. Kuanzia wakati huo mpaka leo sijawahi kumuona.Na Mungu alinisaidia miaka mitatu baadae nilikua tayari na curio shop yangu na nimeweza kujanga kanyumba kakuishina watoto wanasoma shule nzuri,miaka Kumi baadae nimeolewa na mwanaume mwingine na anasomesha wale watoto wake.Story ni ndefu lakini kwa ufupi huu unaweza kupata picha.Ushauri wangu kwa huyu dada, Kwanza naona ni mpiganaji, kwa hakika najua atashinda:Kwanza huyo dada aombe rehema kwa Mungu na atubu kwa yote, maana kabla ya kuolewa na huyo jamaa inawezekana Mungu alikua anamuonya na hakusikia au hakujua. Aombe rehema kwa Mungu. Zaburi 71 iwe sala yake itamsaidiaPili, ajiunge na huduma yoyote kanisani amtumikie Mungu kwa moyo wake wote huku akiomba kwa bidii kwa ajili yake na watoto wake.Tatu Ajitahidi kumfuta huyo jamaa kwenye moyo wake na mawazo yake, amuombe Mungu asiwakutanishe hata njiani Zaburi 35 yote. Aweke maisha yake kwa Mungu na amuombe Mungu ampe Mume wa kweli na siyo mpenzi au rafiki wa MudaAishi Maisha safi ya utakatifu. Siku si nyingi Mungu atakutana nae.Mungu ni mwaminifu, atashangaa jinsi atafanya miujiza na kila kitu kitabadilika bila hata yeye kupambana sana.Mkabidhi Bwana njia zako umtumaini nae atafanya.Let her hold unto God he will never live her alone. Malaika wake watapigana kwa niaba yake. Vita ni vya Bwana.Dada haya ninayokwambia yanatokana na yale niliyoyapita kwenye maisha, na wala sikuwa msomi wala kupata bahati ya kwenda shule kama yeye. Lakini Mungu amenitoa utukufu hadi utukufu.Siwezi kusema yote hapa ila Najua Mungu atamsaidia, Asimfanyie huyo jamaa chochote amkabidhi kwa Mungu.