Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,505
- 4,427
Hali ya wanaCCM kuogopa kujiita wanaCCM kujiita wanaCCM imerudi tena baada ya baadhi ya wanaCCM kwa makusudi kabisa kuamua kunajisi taswira na jina la CCM mbele ya jamii.
Jamii imeanza kupata uelewa na mwelekeo tofauti kwa CCM baada ya aliyekuwa katibu wake was itikadi na uenezi Nape Nnauye kutoa kauli yenye kuashiria nia ovu kwamba "...CCM ina wenyewe..."
Historia ya Nape kisiasa imejaa mashaka na kutoaminika kutokana na kukosa uadilifu. Kuna tetesi Nape katajwa katika ripoti ya dkt Bashiru ya uchunguzi was Mali za CHama kama moja ya watu waliojimilikisha Mali za chama kinyume na utaratibu. Iweje mtu wa hivi aseme CCM ina wenyewe ikiwa nae anajiweka kama hao wenyewe?
Kauli hiyo ya CCM ina wenyewe iliyotolewa na Nape sio tu imenajisi misisngi ya kuasisiwa kwake pia imeweka hofu kwa wote wasio hao wenyewe kama wanaweza kuchaguliwa kuwa miongoni mwa wenyewe. Ziadi ya yote, kauli hiyo inasema kwamba CCM si moja na haiwezi kuwa moja.
Ili kumaliza utata huu ,nawashauri CCM kutumia platform zake ilizo nazo kuanzisha kampeni ya CCM HAINA WENYEWE BALI NI YA WOTE na pia kwa kauli hiyo Nape hatakiwi kuachwa bila kuonywa, kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kuwajibishwa.