Ianzishwe Labour Court of Appeal Tanzania

ThnkingAloud

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2017
Posts
546
Reaction score
564
Serikal ilipoanzisha Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (Commission for Mediation and Arbitration - CMA) na sheria mahususi ya Ajira na Mahusiano Kazini Sura 366 ya mwaka 2019 pamoja na Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi ilikuwa na lengo kuu la kuhakikisha mashauri yanayohusu ajira, wafanyakazi na waajiri yashughulikiwe haraka na kwa gharama ndogo ili mfanyakazi na mwajiri kila mmoja apate haki yake bila kuchelewa.

Changamoto iliyopo kwa sasa ni ucheleweshwaji wa kusikilizwa rufani za mashauri kwenye Mahakama ya Rufaa ya Tanzania. Rufaa zinachukua kwa uchache miaka mitatu kusikilizwa na kuamuliwa na Mahakama ya Rufaa. Wakati mwingine Mahakama ya Rufaa inatengua maamuzi ya Mahakama Kuu na CMA na kuamuru mashauri yasikilizwe upya kuanzia CMA baada ya kubaini maamuzi yao kutolewa kinyume na sheria. Hii inapelekea mashauri kuchukua zaidi ya miaka kumi. Wakati huu wote mfanyakazi anakuwa anahangaika kutafuta haki ambayo kwa utaratibu wa sasa inacheleweshwa na gharama kuongezeka kinyume na malengo ya kuanzisha CMA na Mahakama ya Kuu Divisheni ya Kazi.

Ninaiomba serikali ianzishe Mahakama ya Rufaa ya Kazi (Labour Court of Appeal) itakayoshughulikia rufaa za mashauri ya ajira na kazi TU kupunguza au kuondoa kabisa kucheleweshwa kusikilizwa kwa rufaa za mashauri ya ajira na kazi.
 
Mkuu umeongea kitu kizito sana,Hii hoja umeanza mwaka na Akili kubwa sana,kuchekewesha Haki ya mfanyakazi ni unyanyasaji mkubwa sana, maana huyo mfanyakazi hapati mshahara,wategemezi wanakosa huduma zilizokuwa zikitokewa zinapungua au kukoma kabisa baadhi,Sasa kesi iende miaka 10!Hii sio sawa na ni udhalilishaji mkubwa!Iundwe hiyo mahakama.
 
Back
Top Bottom