Ibada ya kuaga mwili wa TB. Joshua inaendelea muda huu

Ibada ya kuaga mwili wa TB. Joshua inaendelea muda huu

Halafu wabongo wasojua mambo wanakurupuka tu kutwokwa na mapovu bila kujua kucheleshwa kuzikwa kwakwe hakuhusiani na lolote lile ndani ya ulokole wala ukristo, Bali ni tabia tu za watu wa western
Kama tabia na tamaduni za kibagani zinaendelea kulindima katikati ya ukristo, nini mantiki ya Yesu kufa msalabani?
Nini mantiki ya kuwafundisha watu kuishi kikristo?
 
Ibada inaendelea mda huu wageni toka sehemu mbalimbali duniani wamehudhuria, kwa hapa Tanzania inaonyeshwa kupitia wrm TV ya Chief suguye ambayo inapatikana kwenye kisambuzi cha startimes, tuendelea kufatilia ibada hii ya kusherekea maisha yake.

View attachment 1846705
Kweli nashangaa wamemzika na viatu wakati alikuwa hapendi kuvaa viatu
IMG_20210708_222809.jpg
IMG_20210708_222802.jpg
IMG-20210708-WA0012.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini huwa tunaambiwa na walokole kuwa ukiwa ndani ya Yesu, tamaduni za kibagani hazina nafasi tena, sasa hii ya TB Joshua inakuwaje?
Embu tuelezane wapi biblia imeandika mtu akifa azikwe haraka? Kwahiyo ni utashi tu unaotuongoza kwenye kuzika haijarishi utazikwa mapema au late, kwahiyo tuwaachie Nigerians to decide what they want hilo halivunji amri yoyote ndani ya biblia.
 
Ibada kwa wafu haina tofauti na ibada ya sanamu. Kamwe, tena kamwe, mtu hapaswi kuabudiwa hata akiwa hai, sembuse mfu?!

Anayestahili kuabudiwa ni Mungu pekee, na ni kuanzia rohoni maana Mungu ni Roho.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Kitu pekee alichokuja kukifanya kristo ni kuleta utawala wa Mungu nakuondoa utawala wa giza ambao ndo mila pamoja na masheria ya kiyahudi
Duh toka lini mila ikawa dhambi ujue Mila including dressing code, language na vinginevyo so Mila na dhambi ni vitu viwili tofauti
 
Ingekuwa vyema ukataja kifungu cha Biblia ambacho ni ingizo la mila za RC. Tatizo mlilonalo watoto wa Kiprotestanti ni kwamba mnachosimuliwa na baba zenu basi na ninyi mnaanza kusimulia wengine. Baba zenu walilazimika kuwasimulia ninyi hivyo ili wahalalishe kujitenga kwao
Mimi hata siko protestant ila huo ni ukweli ka ibada za sanamu hazikuwepo kwenye bible, na hyo sio RC tu hata Ethiopian church mbona iliingiza vitu vya kitamaduni kwenye taratibu zao za church. Hafu mbona pia makanisa mengi yameingiza agenda za wanadamu.
N. B nimekuwa tu neutral with what I know and understand
 
Embu tuelezane wapi biblia imeandika mtu akifa azikwe haraka? Kwahiyo ni utashi tu unaotuongoza kwenye kuzika haijarishi utazikwa mapema au late, kwahiyo tuwaachie Nigerians to decide what they want hilo halivunji amri yoyote ndani ya biblia.
Jaribu kunisoma vizuri hapo.
Sina tatizo na tamaduni za watu, nina shida na tamaduni za kibagani zinapotangulia imani ya kikristo. Huo utamaduni wa kukaa na maiti muda mrefu huko Nigeria ni utaratibu wa kibagani wa muda mrefu sana. Sio mtindo wa maisha, ni utamaduni rasmi wenye misingi na mizizi kwa imani za jadi huko Nigeria.
Ukristo unasema nini kuhusu maiti?
Ukristo unasema nini kuhusu mazishi?

Badala ya kuja hapa na rejea za imani kikristo kuhusu namna TB Joshua anavyozikwa, wewe unakuja na rejea za tamaduni za kibagani za watu wanaijeria wanavyozika watu wao, mantiki iko wapi?

Kwa mfano, embu waza tu, kiongozi mkubwa wa kidini kama Tb Joshua kukaa mwezi mzima bila kuzikwa huku waumini wake wakimuombeleza, mantiki yake kikristo ni nini?
Ina faida gani kwa kijamii, kiuchumi au kiimani?
 
Walokole watu wa ajabu sana.Ukifiwa wakija kwenye msiba wako utasikia marehemu ameishakufa hiyo ni mifupa hana connection na chochote mkazike wala hakuna kulia.

Angalia sasa wao yamewakuta mpaka leo bado wanazunguka tu na maiti. Si wangemzika tu siku ile ile maisha yaendelee. Yesu alizikwa siku hiyo hiyo na akafufuka siku ya tatu huyu kakaa mwezi sasa wanaendelea kusujudu mzoga
Akifa mwingine wanasema ni dhambi kulia sana,wanasemaga waache wafu wazike wafu wenzao.
 
Ndio maana waislamu hawanaga mambo ya kupeana majonzi muda wote,hapo ukute wenye kutumia fursa kama kulisha wafiwa,mc,mtu wa mampambo nk wanatamani msiba ukae hata mwaka ili waendelee kupiga pesa,kufa kufaana
Arabic culture
 
Kwa mfano, embu waza tu, kiongozi mkubwa wa kidini kama Tb Joshua kukaa mwezi mzima bila kuzikwa huku waumini wake wakimuombeleza, mantiki yake kikristo ni nini?
Ina faida gani kwa kijamii, kiuchumi au kiimani?
Nadhani ilitakiwa wewe unayeona si vizuri ndio uje uelezee kuwa kufanya hivyo kuna ubaya na hasara gani
 
Back
Top Bottom