Ibada ya kusali huku mkizunguka kitu(Circumambulation) ni upagani?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Hii ishu ya kusali mkizunguka kitu ipo karibu katika dini zote kubwa duniani.

Wakristo hufanya hivi. Wakatoliki husali kwa kuzunguka sanamu ya Bikira Maria, Yesu, au mtakatifu mwingine. Huzunguka mara tatu kama ishara ya utatu mtakatifu.

Wabuddha na wahindu na nao husali namna hii ya kuzunguka. Wakizunguka maeneo au vitu vitakatifu.

Waislamu nao wanafanya hivi wakizunguka kaaba. Inasemwa zamani wapagani wa Maka walikuwa wakiizunguka Kaaba wakiwa uchi. Mtume akaja kukataza kitendo cha kuzunguka uchi lakini hakukataza hiyo ibada ya kuzunguka.

Wayahudi nao wana ibada ya kuzunguka. Wao huzunguka kumbukumbu la torati.

Hii ishu siyo upagani kweli?
 
Upegani ndo nini? Ukijubu hilo vizuri utapata jawabu lako haraka
 
Itakuwa Sio upagani
 
Upagani ni nini na features za upagani ni nini?
Mimi mambo ya imani yananifurahisha.
Mwislamu atasema hawa wanabudu mtu na sanamu, halafu mkristo atasema hawa wanaabudu jiwe na eti wanampiga mawe shetani, halafu wote hawa wawili watamsema mhindu anaabudu ng'ombe.
Yani kila mwenye imani hii anamuona mwenye imani ile anachekesha.
🤣😀
 
Imani ya kweli ni upendo. Zingine mapokeo kutoka kwa watu wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…