Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwanza kabisaaa naweza kutoa ushauri mdogo na wa akili ambao mnaomjuwa Richard Mavoko naomba mumfikishie ujumbe na haya ni mawazo yangu kama shabiki yake ambae nilikuwa nafatilia sana nyimbo zake...kwanza kabisaa naweza kusema Rich Mavoko umefanya kosa kubwa sana kujoin WCB kitu ambacho hutokuja kusahau kwenye maisha yako
Kwa nini nasema hivyo nimesema hivyo kwa kwa sababu wewe ulikuvyokuwa unakuja ungeweza kuwa mpinzani wa Diamond kwa kiasi kikubwa sanaa,ok why nasema hivyo kwa sababu nyimbo zako kwa kiasi kikubwa sana zilikuwa zina hit na watu wengi wanazipenda na kukuita Diamond wa pili je swali nini kimekushawishi kuingia WCB??naweza kutoa jibu na kusema kwamba huko WCB nona uwakika wamekutafuta na kukuomba ujoin kwenye rebo yao ili wakumalize kimziki na usizodo kutamba
Nikuambie msemo mmoja unasema kwamba ukiwa unafanya kazi kwa mtu kamwe huwezi kuwa na hela kuliko yeye mwenyewe unaemfanyia kazi hapa namaanisha kwamba kujoin WCB under Diamond ni kwamba kamwe huwezi kuja kufanya mziki ukawa mzuri na kukibalika kumzidi yeye mwenyewe Diamond ambaye ameku sign....kitu kingine ni kwamba Management yako au manager wako atakuwa amekula hongo kubwa kukushauri wewe uingie kule kana kwamba anajuwa anafanya makosaa....
Mziki wako ulikuwa sio wa kujoin kundi lolote au kusainiwa na mtu yoyote wewe ulikuwa ni mwanamuziki wa kipekee ambaye naamini ulikuwa unaji control vizuri sanaa hata kwenye nyimbo zako mwenyewe bila kumshirikisha mtu yoyote yule ulikuwa unafanya vizuri sanaa je nikuulize swali nini ambacho ulikuwa umekosa mpaka kujoin WCB??
Nikutolee mfano angalia huo wimbo ambao umeachia jana je umewahi kuimba nyimbo za design hiyo hata siku moja??je kama upo naomba uwekwe hapa jukwaani....huo wimbo umetoa jana under WCB hata club ukipigwa hamna atakaye amka na kucheza je huo wimbo vile vile unaweza kwenda kwenye show na kuupiga mbele ya mashabiki??
Mimi kama kaka yako nakushauri kwa roho nzuri na kama shida ni hela nipo tayari kukusaidia na kuku support nashauri au nakushauri sikujui na hunijui wala hatuwahi kuonana nakushauri cancel contract endelea kuwa kivyako endelea kutoa vitu vya maana....angala huo wimbo ulitoa jana aalafu uniambie baada ya miezi 2 kama utahit hata kidogo...
Nipo tayari kuku control na kuwa Manager ikiwezekana kwa kipaji chako ulichonacho nipo tayari kuku control kimuziki
Ngoma itasumbua sana hii,sasa hivi ni bado mapema tu na haijazieleka masikioni pa watu...hlf ndo zilivo ngoma za mavoko huwa zinaanza kuhit taratiiibu,mwisho inakuwa ya taifa,binafsi wimbo wake wa pacha wangu nlikuja kuuelewa baadae sn na mpk leo naukubali sna...the same kwa wimbo wa bado wa harmo,kwa mara ya kwanza niliona dogo kazingua ila kadri siku zinavosonga nami nazidi kuuona mtamu!so tuupeni muda na huu,mtauelewa tu.
Sorry unaweza kunitajia nyimbo mbili za mwisho alizotoa Mavoko? Naomba majina ya hizo nyimbo
Uongo huu..angeimba nje ya wasafi mgeisifu..nyimbo nzuri
Nafikiri wewe sio fan wa Rich, ametoa nyimbo mbili kabla ya kujiunga Wasafi na zote hazi kufanya vizuri. Wimbo wake wa mwisho kufanya vizuri ni pacha wangu baada ya hapo akawa anatoa lakini haziskiki mfano Naimani. Huu wimbo ni mzuri mno siku ukiusikiza bila kulinganisha na chochote utaupenda sanaAngalia Rich Mavoko - Pacha wangu alafu angalia na Rich Mavoko - Marry me na zaidi kuna hii ameshirikishwa na Matonya feat Rich Mavoko - Mule mule hizo naweza kusema latest kidogo je unaweza kufananisha na huo ameachia jana tuache ushabiki tuongee vitu vya ukweli
Hii nyimbo Napenda uandishi zaidi!
Hii nyimbo ina uandishi mzuri na ujumbe..Nyimbo za bongo kuna kupenda maandishi kweli??mkuu mbona kidogo unapotea sasa??
Nafikiri wewe sio fan wa Rich, ametoa nyimbo mbili kabla ya kujiunga Wasafi na zote hazi kufanya vizuri. Wimbo wake wa mwisho kufanya vizuri ni pacha wangu baada ya hapo akawa anatoa lakini haziskiki mfano Naimani. Huu wimbo ni mzuri mno siku ukiusikiza bila kulinganisha na chochote utaupenda sana
Hii nyimbo ina uandishi mzuri na ujumbe..
Sio mbaya sana but sio mzuri sana. Kwa level ya mavoko hii nyimbo ni too low. Na kulikuwa na uharaka gani wa kurelease hiyo single mapema hivyo coz member wenzake kwa hiyo level bado nyimbo zao ziko kwenye chati navyojua lebel inakuwa na kitu cha kuachiana mda wa kushusha vitu sio kila siku.
Sasa kwa huu wimbo itabidi afanye kazi sana kwa second single LA sivyo ndo basi tena kwa mavoko.
Sawa nyimbo mbaya mumeianzishia thread na mnatolea mifano ya nyimbo zake zilizopita zilikuwa nzuri, MIMI NAOMBA MTU ALIYEWAHI KUMUANZISHIA THREAD YA KUMSIFIA KWA NYIMBO ZAKE NZURI KABLA YA HII MNAYOSEMA "MBAYA" kama ipo hiyo thread ya kumsifia hapa wekeni tuione, KAMA HAIJAWAHI KUWEPO HIYO THREAD ZA KUSIFIA HIZO NYIMBO MNAZOZISEMA ZILIKUWA "NZURI" BASI JIBU NI KAMA WALIVYOSEMA WENGINE HAPO JUU KWASABABU YUPO WCB. Na kwa sasa mutamjua sana hata anakula nini mutatuletea thread CHEZEA WCB WEWE.
Aje haipotezeki aisee.Ili kuupoteza "aje" ni lazima zitolewe nyinginyingi
Ulikua wapi siku zote mkuu kumsaidia, Muziki unahitaji Management inayojua inanachofanya na Pesa, mnakaa mnakua na Negative thinking bila msaada! Alichofanya Mavoko ni kwa Mustakhabari mzima wa Maisha yake kimuziki, na sio kwa mustakhabari wa Maisha ya Washabiki wa muziki!
Penye ukweli tutasema asee ngoma mbovuuu haivutii bora hata natafuta kiki ya Raymond