Ibara 28 za Tume ya Warioba zilizoondolewa

Hawawezi kuziacha hizi ibara za 15,16,17,18 na ishirini maana ndo zinapingana na Rushwa ambayo ndiyo mshipa wa uhai wao!

Mungu wangu! mbona mambo mazuri ndiyo yamefutwa, kulikuwa na haja gani ya kufuta ibara za 16,18,20 zinazoeleza miiko ya KIONGOZI wa umma.

Je, hili nalo lilikuwa ni MSIMAMO wa CCM kuwa hawatakati Tanzania tupate viongozi wazuri wenye miiko ya uongozi, kama ilivyokuwa msimamo wa CCM kwamba hawataki muundo wa S3?! Kweli CCM ni she.tani na ma.shetani.

Nitaipinga hii rasimu ya 3 ya katiba kwa NGUVU zangu zote, kwa AKILI zangu zote, na kwa UWEZO wangu wangu wote, ili dunia ifahamu kwamba Tanzania hatujawahi kuandika katiba ya wananchi kuliko kukubali huu uj.uha.

CCM hata kwa wale wafia chama kusema kweli mnakatisha tamaa!
 
Hii TZ kila kitu kinawezekana,,maana watanzania ni watu wakarimu na watiifu sana. Tehe tehe
 
WQafungue tovuti ya tume ya Warioba tunataka kuanza uchambuzi ulioenda shule sio huu upuuzi wa prof. Essey anaofagilia sita. Huyu profesa nafikiri ni wa kukaanga sumu pale SUA. Kazoea kucheza na panya na nguruwe sio binadamu.
 

Yote hayo yalijulikana tangu mwanzo wa kutunga sheria ya mabadiliko ya katiba hadi kwenye uteuzi wa wajumbe wa BMK. Cha kufanya ni watanzania kuikataa kabisa na ikibidi tungekataa hata hilo zoezi la kupiga kura maana mwizi ni mwizi tu lazima zoezi zima la kupiga na kuhesabu hizo kura za maoni liwe na wizi ndani yake ili wajitakase kwamba katiba hiyo imeridhiwa na watanzania wengi.

Nafikiri elimu ya kukataa rasimu hiyo iendelee kutolewa kwa juhudi na maarifa zaidi. Maandamano na utaratibu mwingine ufanyike ili kutoa ufafanuzi mwepesi kwa watu wa kawaida juu ya ibara zilizonyofolewa ili waliobarikiwa kuibia wenzao waendelee kufanya hivyo . Mwizi ni mwizi tu na anapokuja kukuibia anakuja na siraha zote, vivyo hivyo hawa jamaa wamejipanga mwanzo hadi mwisho. Mwizi siku zote abembelezwi ni wa kukamata kwa nguvu na kumpa kipigo tu
 
Hivi unategemea jambo zuri kutoka kwa watu wa ccm? Hawa wanajiona hii nchi ni yao na hawategemei kuiachia ndo maana jambo la kitaifa kama hili wanafanya kutimiza matakwa yao. Watanzania hatuhitaji kulalamika sana tunahitaji kuchukua action. Thats all
 
Hivyo vipengele vilivyo ondolewa ni bingo kwa upinzani
ccm wamejianika wanachotaka kiwepo Tanzania na hii inaweza kuwasababishia mathara makubwa kama upinzani wakivinuukuu nakuvitumia vizuri hivi vipengele vilivyo ondolewa.

kuna ambavyo vinagusa maslahi ya wananchi ukiachana na mambo ya muungano mfano ni ule uwajibikaji waviongozi
hiyo nipoint tosha

wala hakuna haja ya maandamano mikutano inatosha
 

Dada yangu hayo ndiyo tunayoyapigia kelele,wala si serikali tatu,kama tatizo lingekuwa serikali tatu basi yale yote yangeachwa likabaki tatizo la serikali tatu.

Lakini tatizo si serikali tatu,tatizo warioba ameminya mianya ya kuiba,kujilimbikizia mali,ubadhirifu,viongozi wabovu,uwajibikaji nk.Haya ndiyo yalikuwa mwiba, na ndiyo maana hawakutaka UKAWA warudi,maana wangeweza wakakubaliana msingi mkubw auachwe yajadiliwe pamoja mengine.

Hawa ndiyo CCM matajiri wenye kila kitu mali yao hata UHAI wetu unategema amri yao,watoto wao,familia zao na rafiki zao.KWa ufupi wafaidikao na ufisadi.
 
Wengine tuliyajua haya toka kipindi kile Celiana Kombani alipokua waziri wa katiba, kitendo cha kusema hakuna haja ya katiba mpya iliyopo inajitosheleza haikua kauli yake bali alitumwa toka magogoni. Ni dhahiri ccm haikua na dhamira ya kweli juu ya mchakato wa katiba mpya ndo maaana mnayaona haya yanayojitokeza sasa. Acha kulia dada yangu, saa ya ukombozi ni sasa.
 
Hao UKAWA si walikimbia sebuleni sasa kusemee chooni ndio nini? MWANAUME WA KWELI HAKIMBII MAPIGANO WALA HAKIMBII NGEDERE WALIOVAMIA SHAMBA LAKE maana ni kuambulia mabua. ndicho UKAWA WANACHOAMBUALIA SASA.
 
Hicho ni kilio cha Umma......tunu za Taifa pia zimenyofolewa,Kiufupi hii ni katiba ya kutubakiza mafisadi madarakani mnaoumwa Njaa mtajua wenyewe Sisi CCM haituhusu.... Ilishasemwa ukitaka mambo yako yakae sawa Njoo upande huu........Rais yupo majuu hana wasiwasi anajua Mr Six na Chenge wanaweza kuongoza Bila yeye kuwapo, mtaimba,mtalia,mtakaa na kusimama lkn katiba ya Sita lazima ipatikane......Mungu ibariki Tanzania.....nimesahau kuwakumbusha kuwa pamoja na roho zetu mbaya ccm lkn pia tunawajali kiaina,si mumemuona Katibu wetu Mkuu akisaidia kajenga nyumba kule kwenye ziara zake........
 
Hapo uliposema hutapiga kura ya maoni umekosea. Kila mtu anatakiwa kupiga kura ya HAPANA kuikAtaa hii rasimu uchwara.
 
sasa wananchi wataamini kwa nini wachache walikataa hiyo rasimu iliyo wasilishwa
 
Pole sana Marry Ngowi lakini nakusikitikia kwa maana UKAWA walipotoka nje ulikuwa hujaelewa wanamaanisha nini hadi jana baada ya mtemi chenge kusoma waraka wa kuwanusuru mafisafi na wazembe!?
Hii pia ni wazi kuwa unaelewa kuwa nchi yetu ni masikini lakini hujui wale wanaosema kuwa ccm wako kwa ajili ya kuendeleza umasikini na wala sio maendeleo. Na bila shaka utakuwa unadanganyika bado na miradi lukuki ya maendeleo lakini mikopo iliyoyafanya hakuna Mtanzania awezaye kuilipa hata kwa miaka 1,000.

 
Hakuna jipya hayo yalijulikana unategemea nini kesi ya nyani,umpelekee ngedere?tutafafakari nini tuwafanye ndio la msingi
 

Umesomeka mkubwa!! hakika hilo ndilo la msingi.
 
Hivi tangu lini mtu anajitengenezea katiba ya kumbana yeye mwenyewe? Ccm walichofanya ndo kinawapa unafuu,Chenge anatuhuma za vijisenti sasa unataka ajiue mwenyewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…