Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,404
- 6,969
Watanzania wengi wanachanganya mambo na kujikuta wakikengeuka na kupotoka.
Ibara ya 1 ya katiba ya JMT inasema wazi kabisa kuwa Tanzania ni dola iliyohuru ambayo ilitokana na kuungana kwa nchi mbili.
Ibara ya 33 (1) imeweka wazi kabisa mkuu wa hii dola na mkuu wa majeshi ni rais wa JMT.
Ibara ya ya 34(1) imetanabaisha wazi kabisa kuwa kutakuwa na serikali ya JMT na kiongozi wake ni rais wa JMT. Na serikali ya JMT itakuwa na majukumu ya kushughulikia masuala yanayohusu muungano na Tanzania bara.
Ibara ya 102 (1) imetamka wazi kuwa kutakuwa na serikali ya mapinduzi Zanzibar ambayo itashughulia masuala ya Zanzibar yasiyohusu Muungano. Kiongozi wake atakuwa ni rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi.
Hivyo basi ni wazi kanisa rais wa JMT anashughulikia masuala ya Muungano na masuala yanayohusu Tanzania bara, huku rais wa Zanzibar anashughurikia masuala ya yanayohusu Zanzibar pekee.
N.b Zanzibar zio dola huru.