Mzee mwenzangu ndio uchovu wenyewe nini maana leo reasoning yako kidogo ina kutu kidogo. Nitachukulia ni majukumu mengi mzee.
Mkuu nijuavyo ni kwamba katiba ya CCM originally iliandikwa na Mwalimu, mwaka 1977
Mzee hili la "ujuavyo" ni vigumu kubishana nalo kwani sijui msingi wa ujuzi wako huo ni nini. Uliona Nyerere akiandika Katiba hiyo, ulisikia Nyerere ndiyo kaandika, ??
Ukiondoa usahihi wa mwaka wa Katiba hiyo nadhani habari nyingine hujazipatia. Ngoja nikupatie tamko lililotolewa na mkutano mkuu wa 1977 wa vyama viwili vya TANU na ASP.
Kwa hiyo basi:-
(1) Sisi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa
pamoja wa TANU na ASP tuliokutana leo
tarehe 21 Januari, 1977 mjini Dar es Salaam,
chini ya uongozi wa pamoja wa Mwalimu Julius
K. Nyerere Rais wa TANU na Ndugu Aboud
Jumbe, Rais wa ASP, kwa kauli moja tunaamua
na kutamka rasmi kuvunjwa kwa Tanganika
African National Union (TANU) na Afro Shirazi
Party (ASP) ifikapo tarehe 5 Februari, 1977, na
wakati huo huo kuundwa kwa Chama kipya cha
pekee na chenye uwezo wa mwisho katika
mambo yote kwa mujibu wa Katiba.
(2) Vyama vya TANU na ASP vinavunjwa kwa
taadhima kubwa. TANU na ASP havikuamua
kujivunja kama vyama kwa kuwa vimeshindwa
kutekeleza jukumu lao. Kwa hakika TANU na
ASP ni Vyama vilivyopata mafanikio ya kipekee
katika Afrika katika kulitekeleza jukumu la
kihistoria na mafanikio hayo ndiyo leo
yamewezesha kitendo hiki cha Vyama viwili
kujivunja vyenyewe. TANU na ASP
vitaheshimiwa siku zote kama viungo muhimu
katika Historia ya Mapambano ya Ukombozi wa
Taifa letu na wa Bara la Afrika, na waanzilishi wa
TANU na ASP watakumbukwa daima kama
mashujaa wa taifa letu waliotuwezesha leo
kupiga hatua hii ya kufungua ukurasa mpya
katika Historia ya Tanzania.
(3) Tumeamua kwa pamoja kuunda Chama kipya
cha kuendeleza mapinduzi ya kijamaa nchini
Tanzania na Mapambano ya Ukombozi wa Afrika
juu ya misingi iliyojengwa na TANU na ASP.
Chama tunachokiunda tunataka kiwe chombo
madhubuti katika muundo wake na hasa katika fikra
zake na vitendo vyake vya kimapinduzi vya kufutilia
kisiasa alitakiwa kuwa ameiandika na Jumbe, aliyekuwa makamu na rais wa Afro Shirazi, I mean that never happened
Tamko la mkutano mkuu limejibu hilo so your "never" is not really "never" for it did happen.
kwa sababu kama Jumbe amngekuwa alishiriki, basi Mwalimu asingekuja kumtema baadaye as he did kutokana na Jumbe kutokubaliana na maamuzi mengi ya mbio mbio ya Mwalimu, ambayo ndio hasa yanatusumbua sasa hivi,
Mzee hii reasoning leo ikoje? Mbona Lowassa katemwa na walikuwa kwenye makubalianao huko nyuma na JK? Watu wanaweza kufanya kazi pamoja leo lakini uko mbele ikabidi waachane, so sioni hii hoja yako nguvu yake iko wapi.
Kama kuna viongozi walishirikiana na Mwalimu, kuandika ile katiba, basi walikuwa ni wasindikizaji tu au hawakuwa na uwezo kabisa wa kufikiri,
Nadhani hicho ni kiwango cha juu cha dharau mzee; maana ningependa kweli kujua majina ya watu wote waliokuwemo kwenye kamati iliyoandika Katiba ya CCM.
maana ukifuatilia maneno the founding fathers wa US, kina Madison, Hamilton, George Washington mwenyewe, utagundua kuwa walikuwa ni watu wenye kuona mbali sana,
Ni kweli waliona mbali lakini siyo mbali kupita Utumwa kwani waliposema kuwa "binadamu wote wameumbwa sawa" hawakumaanisha na watumwa! Lakini hilo haliondoi ukweli wa mchango wao katika mfumo wa Katiba ya sasa na uthibitisho kuwa hata watu wakubwa na mashujaa kama kina Hamilton, Jefferson, Washington na wengine wanaweza kukosea. Nadhani ni sisi tu ambao tunataka kukana kila alichoandika muasisi wa Taifa letu ati kwa sababu "hakuona mbali".
ndo maana huko ma-US hakuna noma kila kitu kipo kwenye sheria,
Mzee kuna noma huku, si unajua kuna mabadiliko mangapi ya Katiba ya Marekani? Je unajua sheria ngapi zimefutwa kwenye mahakama kwa kupingana na katiba?
Katiba ya CCM hata ibadilishwe vipi, siku zote ni lazima ifanane ma mawazo ya Mwalimu,
Si kweli, na kama kuna wana CCM wanaofikiri hawawezi kubadili Katiba yao (kama kukifutilia mbali kipengele hiki) basi wao ni watumwa wa mawazo ya Nyerere. Lakini kama fikra na mawazo ya Nyerere yalikuwa sahihi katika mambo fulani ni ubaya gani kukubaliana nayo au kureflect mawazo hayo? Si leo hii tunajaribu kurudi kwenye miiko ya uongozi na maadili ya uongozi ambayo Nyerere aliyasimamia. Tusifanye hivyo kwa kuogopa kurudi kwenye mawazo ya Nyerere?
we all rememmber maneno aliyokuwa akiyasema 1995, wakati wa kampeni I mean mengine ni aibu hata kuyarudia akisema kuwa CCM ni lazima itawale bongo, upinzani ni good tu for sidelines,
Mzee, Nyerere hakuwahi kusema unayoyasema wewe; Mwalimu alisema kile alichomaanisha, ni kumuwekea maneno ambayo hakuyasema. Naomba unioneshe ushahidi mahali popote ambapo Mwalimua "alisema" kuwa "CCM lazima itawale" Bongo au "Upinzani ni good tu for sidelines". Ukinionesha nitakubali, and believe me I'm a very good student of Mwalimu.
Mrema agombee ubunge tu, mtu ambaye alikuwa deputy Prime minister,
Hapana hakusema "agombee ubunge tu", muulize Mrema akuambie alichosema Mwalimu au angalia ripoti utajua what Mwalimu actually told Mrema na guess what, he was right. Yaani Mrema angekuwa Rais wetu?
I mean my point ni kwamba all in all Mwalimu, ndiye muanzilishi wa haya mawazo ya chama kwanza kuliko taifa, chama kushika hatamu, ili kuondokana na haya mawazo kwanza ni lazima tuanze na ku-denounce yalikotokea, otherwise, tutaendelea kudanganyana tuu!
yawezekana uko sahihi hapo, lakini kama yeye alikuwa ni mwanzilishi basi tumpe credit ni yeye aliyeanza kuyakataa. Lakini pia inasikitisha kuwa hadi leo kuna wana CCM na akili zao timamu ambao bado ni watumwa wanaoogopa kubadili katiba ya CCM kwa vile "iliandikwa" na Mwalimu. Wana CCM hawa ni aibu kwa watu wote wenye fikra huru. Wananikumbusha wale watu-mashine wa Star Trek wenyewe wanajulikana kama "borgs". (pichani)
Ma bogi wanafanya kazi kama "mmoja" na lolote linalomtokea mmoja mwingine analijua kile wanachokiita "hive mind". CCM wako kama hivyo kiasi kwamba wamefungwa na fikra za Chama kiasi kwamba hawaoni kitu kingine chochote kile.
a. Aliwaambiwa CCM siyo "mama" na akamwambia Kawawa kuwa ana ujasiri sana kwa kuapa kuwa atakufa CCM.
b. Aliwakatalia CCM walipoamua kufuata haki ya wananchi kuchaguliwa bila chama na akaweka haki za raia mbele wakati CCM imebadili Katiba kuzuia hilo, na hadi leo hakuna kiongozi yeyote wa CCM ambaye amepingana na chama chake kuhusu hilo isipokuwa alivyofanya Nyerere.
c. Ni Nyerere aliyekuwa tayari kurudisha kadi ya CCM wakati wamemtumia ujumbe wale jamaa wa kumtetea Lowassa.
Mwalimua aliiweka CCM mbele pale tu CCM ilikuwa inaitumikia nchi kwanza lakini naamini kwa mishipa ya damu yangu yote, kama Mwalimu angekuwepo na kuona waliyoyafanya kina Mkapa, JK na ukimya wa vigogo wengine wa CCM, angerudisha kadi jangwani!! Hakuwa anajikomba kwa mtu yeyote ndani ya CCM.