Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naoana Waheshimiwa mnajadili TEXT ya ibara hiyo badala ya CONTEXT!
You are very clever!
Wasababishaji wa matatizo yetu ni sisi wenyewe...
CCM kama chama kilichopewa dhamana ya kuongoza Tanzania, tulitegemea kuanzia kwenye katiba yake ingekuwa na lengo hilo hilo liwe msingi wake nambari moja.....kulitumikia Taifa letu kwa moyo mmoja.
Kumbe tumewaweka madarakani watu ambao maslahi yetu yanakuja baada ya yakwao??
Hivi na katiba za vyama vingine (CHADEMA, CUF etc) zikoje?? usikute nako kuna huu utumbo...
Nionesheni nchi yenye Katiba mbaya na imeendelea na nitawaonesha nchi yenye katiba mbovu na haijaendelea. Huwezi kuwa na Katiba mbovu ukategemea maendeleo, lakini ukitengeneza Katiba nzuri unafungulia msingi wa maendeleo..
Wakuu hiyo katiba ya CCM ilibuniwa na kuandikwa na Mwalimu mwenyewe, sasa hatuhitaji spin kwenye hili sasa kama hii katiba ya CCM ndio chanzo cha taifa letu kudumaaa kimaendeleo, then there you go,
Otherwise, matatizo yetu ni sisi wenyewe wananchi na viongozi, hapa tulipofikia hakuna wa kumlamu zaidi yetu sisi wenyewe, sasa ungetegemea by sasa tuwe tunajaribu ku-get things right wapi, ndio kwanza tunaiilia katiba ya CCM, ambayo hata Mwalimu mwenyewe never respected it.
He only did things his ways, sasa nashangaa kwamba hata hatuelewi kuwa maneno ya kuweka chama cha siasa mbele kuliko taifa, hatuelewi yaliwekwa na nani,
Wakati Mwalimu, anampigia debe Mkapa kuwa rais, hivi mnakumbuka exactly maneno aliyokuwa akiyasema, ni haya haya ya kuweka CCM mbele kabla ya taifa, sasa kama wameamua kuyaenzi basi we are dooomed! Haya maneno ya katiba ya zamani yalikuwa goood only kwa nidhamu tu ya viongozi, lakini hayakutuletea maendeleo ya taifa, meaning kwamba ni wakati muafaka sasa wa kuachana nayo na kurudi kwenye utawala wa kuheshimu sheria za jamhuri.
Katiba ya makaburu wakati wa Apartheid...
Upande gani? unanionesha Katiba mbovu na nchi iliyoendelea, au Katiba nzuri na nchi isiyoendelea..?
Separate but equal...hiyo haikuwa kwenye katiba? Kama ilikuwepo kwenye katiba basi hiyo katiba ilikuwa mbofu lakini uchumi wa nchi (kwa ujumla) uliweza kushamiri.
mzee nilisema wapi kuwa Katiba nzuri inahusiana na uchumi mzuri?
Unaposema maendeleo unamaanisha nini sasa?
Wewe ndio umesema huwezi kuwa na katiba mbovu na ukategemea maendeleo...niambie basi hayo maendeleo kwako ni yapi....
Nyani, nilidhani muda wote huu utakuwa umeelewa mawazo yangu kuhusu maendeleo; maendeleo ni ya watu na si vitu. Katiba nzuri inaendeleza watu siyo vitu. Yaani, vitu vinatumika kuendeleza watu na hapa watu nina maana jamii nzima ya watu wa nchi ile na siyo kikundi kimoja cha watu.
Kwa hiyo basi katiba ya Marekani nayo sio nzuri maana kuna idadi kubwa ya raia wake ambao hawana maendeleo. Leo nimesikia redioni kuwa katika kila sekunde 29 kuna mwanafunzi wa high school ana drop out! Hapa nilipo kwa mfano ni asilimia 44 tu ya wanafunzi wa high school wanaomaliza mafunzo. Hii ni asilimia chini ya hamsini! Kwa mtaji huo basi hata katiba ya Marekani si nzuri...hasa ukiangalia mambo mengine kama welfare, teenage pregnancy, idadi ya watu wanaoishi chini ya mstari wa umaskini n.k.....
Hicho kifungu in question kiliandikwa/ kiliwekwa lini kwenye hiyo katiba ya CCM?
Mzee, walioshiriki kuandika Katiba ya CCM wanajulikana mmoja wao ndio aliyesoma maazimio ya CCM Butiama. Nyerere hakukaa chini kubuni na kuandika Katiba hiyo.
Mkuu nijuavyo ni kwamba katiba ya CCM originally iliandikwa na Mwalimu, mwaka 1977
kisiasa alitakiwa kuwa ameiandika na Jumbe, aliyekuwa makamu na rais wa Afro Shirazi, I mean that never happened
kwa sababu kama Jumbe amngekuwa alishiriki, basi Mwalimu asingekuja kumtema baadaye as he did kutokana na Jumbe kutokubaliana na maamuzi mengi ya mbio mbio ya Mwalimu, ambayo ndio hasa yanatusumbua sasa hivi,
Kama kuna viongozi walishirikiana na Mwalimu, kuandika ile katiba, basi walikuwa ni wasindikizaji tu au hawakuwa na uwezo kabisa wa kufikiri,
maana ukifuatilia maneno the founding fathers wa US, kina Madison, Hamilton, George Washington mwenyewe, utagundua kuwa walikuwa ni watu wenye kuona mbali sana,
ndo maana huko ma-US hakuna noma kila kitu kipo kwenye sheria,
Katiba ya CCM hata ibadilishwe vipi, siku zote ni lazima ifanane ma mawazo ya Mwalimu,
we all rememmber maneno aliyokuwa akiyasema 1995, wakati wa kampeni I mean mengine ni aibu hata kuyarudia akisema kuwa CCM ni lazima itawale bongo, upinzani ni good tu for sidelines,
Hapana hakusema "agombee ubunge tu", muulize Mrema akuambie alichosema Mwalimu au angalia ripoti utajua what Mwalimu actually told Mrema na guess what, he was right. Yaani Mrema angekuwa Rais wetu?Mrema agombee ubunge tu, mtu ambaye alikuwa deputy Prime minister,
I mean my point ni kwamba all in all Mwalimu, ndiye muanzilishi wa haya mawazo ya chama kwanza kuliko taifa, chama kushika hatamu, ili kuondokana na haya mawazo kwanza ni lazima tuanze na ku-denounce yalikotokea, otherwise, tutaendelea kudanganyana tuu!